Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:ACHILEUSGNICHOLAUS/sandbox

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
          KICHWA: SIKU YA KWANZA KUTUMIA SIMU MAHILI(SMART PHONE)
Muhtasari:

Kwa miaka mingi, teknolojia ya simu mahiri imekuwa ikikua kwa kasi, ikigeuza njia tunavyoishi na kufanya kazi. Kwa bahati mbaya, nilikuwa nimechelewa kuingia katika ulimwengu huu wa kuvutia wa simu za mkononi zenye uwezo mkubwa. Lakini siku hiyo ya kipekee, niliamua kufanya mabadiliko.

Kuanzishwa kwa Simu Mahiri:

Ninapoangalia nyuma, siku hiyo inaonekana kama mwanzo mpya. Nilipokuwa nikifungua kifurushi changu kipya cha simu mahiri, nilihisi mchanganyiko wa msisimko na wasiwasi. Nilikuwa na hamu ya kujifunza na kuelewa jinsi teknolojia hii ingeathiri maisha yangu ya kila siku.

Kugundua Uwezo Mpya:

Baada ya kufunga simu yangu mpya na kuanza kuitumia, niligundua ulimwengu mpya wa fursa na uwezekano. Kamera bora, programu za kusisimua, na uwezo wa kuunganika na ulimwengu kupitia mitandao ya kijamii zilinivutia sana.

Mashaka na Changamoto:

Hata hivyo, safari hii haikuwa bila changamoto. Kutumia teknolojia mpya kwa mara ya kwanza kulikuja na mchakato wa kujifunza na kuzoea. Nilipata shida za kujaribu kuelewa mifumo ya uendeshaji na programu mbalimbali. Lakini kwa kujitolea na uvumilivu, nilianza kuona maendeleo.

Uamuzi wa Kujifunza:

Changamoto hizi zilinifanya niamue kujifunza zaidi kuhusu teknolojia ya simu mahiri na usalama wa mtandaoni.Nilianza kuwa msumbufu wa hali ya juu kwa marafiki zangu wa karibu maana baadhi yao walikua wakitumia hizo simu kubwa.Niliendelea kuwa mchokozi nikijaribu kujifunza vitu vingi zaidi na nikaendelea kupata ujuzi mwingi kadri siku zilivyozid kusogea.

Siku baada ya siku:

Siku zilizofuata, nilikua nikiamka nimejaa shauku ya kugundua zaidi kuhusu simu yangu maana ilikua bado ni kitu kipya akilini mwangu. Nilianza kwa kuchart sana, kupiga na kudownload miziki, kupiga picha nyingi nyingi na kucheza magame ambayo nilidownload.Na hayo yote ilikua ni furaha tu ambayonilikua nayo baada ya kuonanaimiliki hiyo simu.Siku ziliendelea kusogea na nikazidi kuwa mzoefu wa kutumia simu japo haikua katika kiwango cha kujiita fundi kama nilivyosaivi, kwamaana kuna baadhi ya vitu sikua najua kuvitumia bado.

Niliamua kujaribu baadhi ya programu za kijamii ambazo nilikuwa nimezisikia. Niliunda akaunti mpya kwenye Instagram na Twitter, nikifurahia kuunganishwa na marafiki na familia yangu mtandaoni. Nilianza kufuata watu(following) na kurasa za kuvutia, nikigundua mada mpya na habari za kusisimua.

Baadaye, niliamua kutumia simu yangu kwa madhumuni ya kielimu. Nilipakua programu za kujifunzia lugha mbali mbali kama C++ kwa sababu pia sikua na PC kwa mda huo, japo ilikua moja kati ya changamoto nilizokutana nazo, kwamaana haikua rahisi kuweza kufanya programming kwa kutumia simu nahivyo ikapelekea kufanya maamuzi mengine ya kununua PC. Kila ilipofika jioni nilipenda kuwashamiziki nakuanza kusikiliza, na zaidi nilipenda sana kuwasha data zangu na kuingia kwenye mitandao ya kijamii ambayonilikua tayari nimefungua akaunti zake kwaajili ya kuangalia vichekesho na stori nyingine nyingi za mitandaoni.

Changamoto Mpya:

Hata hivyo, sikuweza kuwa mtumiaji mzuri wa simu kubwa bila ya kupata changamoto nyinginezo kwa sikuzilizofuata. Changamoto zilikua kama ifuatavyo:

1.Nilipoteza muda mwingi sana wakati wa kujifunza.

2.Nilipoteza sana hela ya kununua vocha kwa ajili ya data ambazo nilizitumia bila kua na mpangilio.

3.Changamoto zaidi ilikua wakati wakuandika vitu mfano messages nilipatasana shida kwasababu nilikua sijazoea.

Hitimisho:

Hata hivyo nashukuru sana kwa maana nimekua mmoja wa watumiaji mahili wa simu kubwa(simu mahili) iliotokana na ukuaji wa utandawaza, nimengi ya zamani yanapotae na mengi mapya yanaingia nakuongezeka katika ulimwengu wa kitekinolojia ambayo mpaka sasa yamepelekea mimi kufahamu matumizi mbalimbali ya tekinolojia, kwamaana mpaka sasa so matumizi ya simu tu bali hadi matumizimengine mengi ya vifaa vya kielectroniki naweza kutumia, kutokana na ujuzi nilioupata zaidi hasa katika elimu yangu ya chuo kikuu cha Dodoma nikiwa katika ndaki ya elimu ya sayansi angavu.