Mto Mwekundu
Mandhari
Mto Mwekundu ni mto mkubwa wa Vietnam ya Kaskazini. Inaanzia katika jimbo la Yunnan la China na kupita sehemu ya kaskazini ya Vietnam hadi kuishia katika Bahari ya Kusini ya China. Urefu wake ni km 1149. Tawimto kubwa ni Mto Mweusi.
Hanoi mji mkuu wa Vietnam iko kando la Mto Mwekundu. Maji yake huwezesha kilimo cha mpunga katika tambarare za Vietnam ya Kaskazini.