Msumenomashine wa kusukuma na kuvuta
Mandhari
'Msumenomashine wa kusukuma na kuvuta (kutoka Kiingereza "push and pull" au "reciprocating") ni kifaa chenye meno cha kukata vitu mbalimbali kama chuma, bomba, misumari, n.k. Meno yake hukata kwa mwendo wa kusukuma na kuvuta (kurudia). Kifaa hiki hutumiwa sana kwenye kazi za ujenzi, huduma za uokoaji na bomoabomoa.
Meno yake ni ya aina mbalimbali kutokana na matumizi yake. Kwa mfano, kuna meno ya kukata chuma, meno ya kukata mbao, meno ya kukata kuta kavu, n.k.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Je ni nani aligundua msumeno huu? Ilihifadhiwa 24 Oktoba 2017 kwenye Wayback Machine.
- Jinsi ya kupata msumenomashine wa kusukukama na kuvuta bora kwa mwaka 2017 Ilihifadhiwa 12 Oktoba 2017 kwenye Wayback Machine.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |