Nenda kwa yaliyomo

Msondo Ngoma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Msondo Ngoma Music Band)
OTTU Jazz Band (au NUTA Jazz Band, Juwata Jazz Band)
Asili yake Tanzania
Aina ya muziki Dansi
Miaka ya kazi 1964 - hadi leo
Wanachama wa zamani
Hassan Rehani Bitchuka
Moshi William
(amefariki)
Muhiddin Maalim
(amefariki)
Saidi Mabera
(amefariki)

'Msondo Ngoma Music Band (zamani NUTA Jazz Band, Juwata Jazz Band kisha OTTU Jazz Band) ni bendi kongwe na maarufu ya muziki wa dansi kutoka nchini Tanzania.

Bendi ilianzishwa mnamo mwaka wa 1964. Wanamuziki mashuhuri wa OTTU Jazz Band ni Joseph Lusungu, Mnenge Ramadhani Muhiddin Maalim, Hassan Rehani Bitchuka, Saidi Mabera na Moshi William.

Bendi hutegemea "National Union of Tanzania" ("Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania" kwa Kiswahili, baadaye "Organization of Tanzanian Trade Unions"); na tokea hapo iliitwa "NUTA", baadaye "Juwata" na baadaye tena "OTTU" kisha Msondo Ngoma ambayo hadi leo inaitwa hivyo.

Leo hii sehemu kubwa ya waimbaji na watunzi mahiri wa Msondo Ngoma wamefariki ikiwa ni pamoja na TX Moshi, Joseph Mahina, Suleiman Mbwembwe, Athumani Momba, Muhidin Maalim Gurumo na Saidi Mabera ambao ndio walikuwa wanatingisha katika bendi hii.

Msondo Ngoma ni miongoni mwa bendi zilizotingisha sana katika miaka ya 1980 na 1990 hadi kifo cha TX Moshi ambaye inasemekana ndiye aliyekuwa mtunzi mkubwa kabisa. Kwa kwenda mbali zaidi, inasemekana katika albamu moja, basi TX anaweza kutunga nyimbo 8 hadi 9 wakati zilizobaki zinatungwa na jumuia. Ipo imani ya kwamba tangu umauti umfike TX bendi ilipungua kasi na ndipo mfululizo wa vifo vya wanachama wengine vikaendelea kutokea mfululizo.

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Msondo Ngoma kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.