Msaada:Vyanzo
Vyanzo ni jambo la kimsingi kwa makala zetu. Anayeleta mada hapa na kuunda makala anatakiwa kuonyesha ukweli wa habari kwa kutaja vyanzo vya habari.
Kutaja vyanzo kunasaidia kuonyesha ya kwamba habari unazoleta ni kweli. Pia kunathibitisha kwamba mada ya makala ina umaarufu wa kutosha ili kustahili kuwa na makala katika wikipedia.
Katika wikipedia vyanzo hivi vinatakiwa kuonekana maana habari zisizo na vyanzo kuna uwezekano mkubwa wa kuondolewa.
Katika wikipedia yetu mara nyingi si rahisi kuonyesha vyanzo kwa sababu wachangiaji wengi hawana nafasi ya kutumia maktaba mazuri penye majarida na vitabu vya kitaalamu.
Kwa hiyo tutatumia mara nyingi vyanzo visivyo vya Kiswahili hasa Kiingereza. Ni sawa kunakili orodha ya vyanzo kutoka makala ya en:wikipedia. Kuna pia vyanzo vizuri vinavyopatikana mtandaoni.
Vyanzo vinavyokubalika, vyanzo visivyokubalika
Chanzo kizuri ni chanzo (kitabu, makala katika jarida, gazeti, intaneti) kinachoonyesha elimu nzuri kuhusu mada yako. Bora kama imetungwa na mtaalamu (ikiwezakana mwenye sifa za kichuo). Ila si rahisi kuipata kwa Kiswahili, mara nyingi tutatumia za Kiingereza.
Kisichokubalika
- makala nyingine ya wikipedia si chanzo. Usitaje Wikipedia ya Kiingereza kama chanzo! Lakini unaweza kuangalia vyanzo vilivyotajwa huko, kwa mfano kunakili tanbihi ya enwiki.
- wakati wote marejeo ya kibiashara ni marufuku, kwa mfano tovuti zinazolenga kutangaza bidhaa
- Kurasa za Facebook na social media (kama Jamii Forums) hazifai.
- Tovuti ya mwenyewe (personal homepage) haifai.
Hizi zote haziwezi kushuhudia msingi wa makala, wala ukweli wala umaarufu.
Unaweza kutoa habari za nyongeza kwenye mitandao ya kijamii kama umeshaweka msingi kwa kutaja marejeo kwenye chanzo kinachokubalika.
Namna ya kutaja vyanzo
- Kutaja marejeo katika kitabu: Utataja jina la mwandishi, jina la kitabu, mwaka wa kuchapishwa na mahali pake, kampuni ya kuchapisha, ukurasa au kurasa penye habari unazorejelea
- Kutaja marejeo katika gazeti au jarida: utataja jina la mwandishi (kama lipo), kichwa cha makala, jina la gazeti/Jarida, tarehe yake
- Kutaja marejeo kutoka intaneti: utataja jina la mwandishi (kama lipo), kichwa cha makala, jina la tovuti, tarehe yake, unaongeza tarehe ulipoangalia tovuti, URL (=anwani ya intaneti). Huwezi kutumia tovuti yoyote. Facebook, twitter na "social media" kwa jumla si vyanzo vinavyofaa kuunda umaarufu au umuhimu wa habari.
- >>Hapo uko huru kunakili marejeo kutoka Wikipedia nyingine; wakati mwingine inawezekana kufungua ukurasa wa wikipedia penye tanbihi katika hali ya "hariri chanzo" na kunakili tanbihi yote; ukiwa kwenye mtazamo wa "hariri" unafungua tanbihi pekee kwenye enwiki, kuinakili, halafu kuingia katika makala yako ya Kiswahili hali ya "Hariri" , bofya "Cite" halafu "Basic" na mwaga yote humo.
Tanbihi chini ya ukurasa
Njia nyepesi kuonyesha chanzo cha habari ni tanbihi (footnotes) chini ya ukurasa. Hapa kuna alama kwenye menyu ya uhariri.
Ukibofya hapa unapata dirisha la .
Sasa andika chanzo au maelezo mengine katika nafasi yake chini ya maneno "Maandishi ya marejeo".
Bado hatua moja: chini ya makala mwishoni kabla ya interwiki andika:
- ===Marejeo=== <references/>
na vyanzo ulivyotaja kwenye mabano au maelezo vitaorodheshwa hapo.
Kama chanzo chako ni tovuti ya intaneti (nje ya wikipedia) fanya hivyo:
- weka kiungo cha nje kwa kuandika mabano mraba [ ] - mara moja tu, si mara mbili jinsi ilivyo kwa viungo kwa makala mengine ya wikipedia!. Kati ya mabano haya unaingiza anwani ya intaneti (unaweza kutaipu pia)
- [http://www.example.com] jina la kiungo
- andika anwani ya tovuti kati ya mabano mraba, acha nafasi tupu 1,2 kabla ya mabano ya pili halafu ongeza maneno ya maelezo
- [http://www.example.com Maelezo yanayoonekana]
Usitaje makala mengine ya wikipedia kama chanzo lakini unaweza kunakili vyanzo kutoka huko KAMA VINAFAA.
Viungo vya Nje
Makala mengi ya wikipedia huwa na sehemu mwishoni inayoitwa "Viungo vya Nje".
Hapa tunaweka viungo vya Nje kwa tovuti zenye maana na kukubalika zinazohusu kichwa na yaliyomo ya makala..
Inatosha kutaipi anwani kamili ya tovuti unayotaka kurejea: