Msaada:Hamisha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wakati mwingine makala ilipewa jina ambalo halifai.

Jina la makala hii lina kosa ("Choo" badala ya "Chuo")
Ufuate hatua hizo ukitaka kuhamisha makala

Ukiona jina tofauti lingekuwa afadhali, unaweza kuihamisha.

Ni afadhali ukiweza kuwasiliana na mwingine aliyetunga au kusahihisha makala hiyo.

Pengine jina liliandikwa kwa makosa. Ukiwa na uhakika, hamisha tu.

Hapo angalia juu ya makala kwenye menyu ya juu.

Bofya "Zaidi" kwenye menyu ya juu. Chagua "Hamisha"

Katika ukurasa angalia chini ya "Kichwa cha habari kipya:" - hapa bofya pembetatu ndogo.

Halafu uandike jina la makala mpya upande wa kulia badala ya lile lililopo.

Hatimaye bofya chini "Hamisha Ukurasa".

Tazama pia

Ukitaka kuhamisha makala kutoka nafasi ya mtumiaji (userspace), angalia hapa Msaada:Jaribio.