Skeli ya ugumu ya Mohs
Skeli ya ugumu ya Mohs (skeli ya Mohs) ni skeli ya kupima ugumu wa madini iliyobuniwa na Friedrich Mohs, mtaalamu wa madini kutoka Ujerumani. Mohs alibuni skeli yake inayofafanua ugumu wa madini ikilinganisha jinsi madini ya aina moja yanavyoweza kukwaruza mengine.
Miamba huundwa na madini ya aina moja au zaidi. Kulingana na skeli ya Mohs, ulanga ni laini kabisa: inaweza kukwaruzwa na madini mengine yote. Jasi ni ngumu zaidi: inaweza kukwaruza ulanga lakini si kalsiti (kabonati ya kalisi, calcite), ambayo ni ngumu zaidi. Madini magumu kabisa ni almasi (diamond) ambayo haiwezi kukwaruzwa na kitu kingine chochote.
Skeli ya Mohs inatumia madini kumi kwa kulinganisha ugumu. Hayo ni ulanga, jasi, kalsiti, fluoriti, apatiti, felspa, kwazi, topazi, korundi (mfano rubi), hatimaye almasi.
Skeli ya Mohs iliundwa miaka mingi iliyopita, hivyo si kamili kabisa, lakini wanajiolojia bado wanaitumia kwa sababu ni rahisi kutumika, hasa kwa utafiti nje ya maabara. Ndani ya maabara kuna pia vifaa vinavyoruhusu kupima ugumu halisi.
Ugumu wa Mohs | Madini | Fomula ya kikemia | Ugumu halisi [1] | Picha |
---|---|---|---|---|
1 | Ulanga | Mg 3 Si 4 O 10 (OH) 2 | 1 | |
2 | Jasi | ZABURI 4 · 2H 2 O | 3 | |
3 | Kalsiti | CaCO 3 | 9 | |
4 | Fluoriti | CaF 2 | 21 | |
5 | Apatiti | Ca 5 (PO 4 ) 3 (OH -, Cl -, F - ) | 48 | |
6 | Felspa | KAlSi 3 O 8 | 72 | |
7 | Kwazi | SiO 2 | 100 | |
8 | Topazi | Al 2 SiO 4 (OH -, F - ) 2 | 200 | |
9 | Korundi | Al 2 O 3 | 400 | |
10 | Almasi | C | 1600 |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Applied Mineralogy: applications in industry and environment. Swapna Mukherjee 2011
Tovuti nyingine
[hariri | hariri chanzo]- http://www.mineraltown.com/infocoleccionar/mohs_scale_of_hardness.htm
- Jinsi ya kutumia kiwango cha Mohs cha ugumu wa madini Archived 30 Desemba 2006 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Skeli ya ugumu ya Mohs kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |