Nenda kwa yaliyomo

Mlipuko wa Dellys wa mwaka 2007

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mlipuko wa Dellys wa mwaka 2007 ulitokea tarehe 8 Septemba 2007, ambapo watu wasiopungua 30 waliuawa na 47 kujeruhiwa katika shambulio la bomu la gari la kujitoa mhanga katika kambi ya jeshi la majini la Algeria katika mji wa Dellys, kilomita 100 (maili 62) mashariki mwa Algiers. Mlipuko huo ulifanywa na washambuliaji wawili ambao waliuawa wenyewe katika shambulio hilo.

Tawi la Al Qaeda kaskazini mwa Afrika (Al-Qaeda Organization in the Islamic Maghreb) ilidai kuhusika na shambulio hilo la kujitoa mhanga.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Al-Qaeda claims Algerian bombings retrieved September 10, 2007