Mkutano wa Kimataifa kwa ajili ya Watoto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mkutano wa Kimataifa kwa ajili ya Watoto ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa ulifanyika katika makao makuu yake yaliyopo New York City, Marekani tarehe 29 - 30 Septemba 1990. Mkutano huu ndio uliokuwa na mkusanyiko mkubwa wa wakuu wa nchi mbalimbali waliojikita katika kutimiza malengo ili kuboresha ustawi wa watoto duniani kote mpaka kufikia mwaka 2000. Hii ndio ilikua mara ya kwanza kwa Umoja wa Mataifa kuweka ajenda iliyolenga kufikia malengo ya kiafya, elimu, lishe bora na haki za kibinadamu. Matokeo mkubwa ya Mkutano huu yalikuwa ni kusaini tamko la Dunia nzima juu ya kulinda, kusimamia na kuendeleza watoto ikijumuishwa na maelezo ya kina juu ya maendeleo ya watoto kwa mwaka 2000. Mkutano huu wa Dunia uliweka umuhimu wa muongozo utakaojikita katika kukuza na kusimamia masuala yote yanayowahusu watoto duniani kote na iliweka umuhimu wa Umoja wa Mataifa kuwa na mikutano mikuu itakayoongelea ongezeko la watu, mazingira, chakula, haki za binadamu, maendeleo ya jamii na haki za wanawake.

Chimbuko la mradi huu[hariri | hariri chanzo]

Mkutano huu ulipendekezwa na Waziri Mkuu wa Canada Brian Mulroney, Rais wa Misri Hosni Mubarak, Rais wa Mali Moussa Traoré, Rais wa Mexico Carlos Salinas de Gortari, Waziri Mkuu wa Pakistan Benazir Bhutto, na Waziri Mkuu wa Sweden Ingvar Carlsson. Viongozi hawa wakubwa sita walifanya kazi pamoja ili kuleta na hamasa na kutangaza kujitolea huko katika ngazi za kisiasa ili kuhakikisha malengo na mipango sahihi inafatwa ili kulinda, Kuendeleza na kukuza watoto kama alama kuu ya maendeleo katika jamii na kiuchumi nchini kote. Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa Javier Perez de Cullar alipitisha mradi huo na aliupa mkutano ushirikiano wa UNICEF na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa. Jumla ya serikali 159 zilialikwa katika tukio hilo. Na walioshiriki ni viongozi 72 kutokea Mataifa tofauti, pamoja na wawakilishi wa nchi 87.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]