Nenda kwa yaliyomo

Missouri (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Missouri River)
Mto Missouri
Ramani ya beseni ya Missouri

Mto Missouri ni mto mkubwa wa Marekani na tawimto muhimu zaidi la Mississippi. Ni mto mrefu kushinda ule wa Missisippi na ni mto mrefu katika Amerika ya Kaskazini.

Chanzo cha mto kipo kwenye milima ya Rocky Mountains katika jimbo la Montana. Missouri inaendelea kupita majimbo ya North Dakota, South Dakota, Iowa, Nebraska, Missouri na Kansas.

Inaishia katika Missisippi karibu na mji wa Saint Louis, Missouri.