Methazolamidi
Methazolamidi (Methazolamide), inayouzwa kwa jina la chapa Neptazani (Neptazane) pamoja na zingine, ni dawa inayotumika kutibu shinikizo la ndani ya jicho (IOP) ikijumuisha glakoma.[1] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.[1] Madhara yake huanza ndani ya masaa manne na hudumu hadi masaa kumi na nane. [1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kufa ganzi, matatizo ya kusikia, uchovu, kichefuchefu, kuhara, na kuhisi usingizi.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha ugonjwa wa Stevens-Johnson.[1] Ni kizuia anhidrasi cha kaboni ambayo hupunguza kutengenezwa wa majiaji yasiyo na rangi yaliyo sawa na plazima ya damu lakini yenye viwango vya chini vya protini (aqueous humor).[1]
Methazolamidi iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani katika miaka ya 1950.[1][2] Nchini Marekani, vidonge 60 vya miligramu 50 hugharimu takriban dola 125 kufikia mwaka wa 2021.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Methazolamide Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 17 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Supuran, Claudiu T.; Nocentini, Alessio (17 Julai 2019). Carbonic Anhydrases: Biochemistry and Pharmacology of an Evergreen Pharmaceutical Target (kwa Kiingereza). Academic Press. uk. 271. ISBN 978-0-12-816745-8. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Novemba 2021. Iliwekwa mnamo 17 Novemba 2021.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Methazolamide Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Novemba 2016. Iliwekwa mnamo 17 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Methazolamidi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |