Nenda kwa yaliyomo

Megatani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Megatoni)

Megatani ni kipimo kinachotaja milioni 1 za tani.

Tani ni kipimo cha SI cha masi.

Mara nyingi hutumiwa kwa kutaja nguvu ya mlipuko wa bomu la nyuklia. Mlipuko mkubwa kabisa wa bomu la nyuklia katika historia ilitokea mwaka 1961 kwenye kisiwa cha Novaya Zemlya nchini Urusi na nguvu ilikuwa megatani 50, yaani sawa na nguvu ya tani milioni 50 za kilipukaji aina ya TNT.