Novaya Zemlya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Novaya Zemlya duniani, pamoja na mahali pa mlipuko wa bomu ya nyuklia
Ramani ya Novaya Zemlya (kiingereza)

Novaya Zemlya (kwa Kirusi Но́вая Земля́, yaani Nchi mpya) ni funguvisiwa la Urusi lililopo kwenye Bahari Aktiki. Eneo lake ni kilomita za mraba 90,650. Kiutawala ni Wilaya ya Novaya Zemlya katika mkoa wa Arkhangelsk Oblast. [1].

Mwaka 2010 ilikuwa na wakazi 2,429 na kati yao karibu 2,000 waliishi katika mji wa Belushya Guba, makao makuu ya wilaya.

Wakazi asilia walikuwa wawindaji na wavuvi wa kabila la Wanenets waliohamishwa kutoka visiwa katika miaka ya 1950 [2]. Wakati ule walikuwa watu wasiozidi 300. [3]. Uhamisho huo ulisababishwa na mipango ya kutumia visiwa kwa shughuli za kijeshi na majaribio ya kulipua mabomu ya nyuklia.

Novaya Zemlya kuna visiwa viwili vikubwa vinavyotenganishwa na mlangobahari mwembamba wenye upana wa mita 600 hadi kilomita chache.

Mlima mkubwa uko kwenye kisiwa cha kaskazini wenye kimo cha mita 1,547.

Hadi leo Novaya Zemlya ni kituo cha kijeshi na wakazi wengi ni wanajeshi pamoja na familia zao. Umoja wa Kisovyeti ulitumia visiwa kwa milipuko ya majaribio ya mabomu ya nyuklia; tarehe 30 Oktoba 1961 mlipuko mkubwa wa kinyuklia katika historia ulitekelezwa hapa. Nguvu ya bomu ilikadiriwa kuwa na megatoni 50.

Mazingira[hariri | hariri chanzo]

Kijiolojia Novaya Zemlya ni endelezo la safu ya milima ya Ural.[4]. Uso wa nchi ni ya milima.[5]

Kisiwa cha kaskazini kuna barafuto nyingi, kisiwa cha kusini kinafunikwa na tundra.[6]

Maliasili ni pamoja na shaba, plumbi na zinki.[6]

Novaya Zemlya inatenganisha bahari za pembeni za Bahari ya Barent na Bahari ya Kara.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sheria ya Urusi #65-5-OZ
  2. Microsoft Word - North Test Site _FINAL_.doc (PDF). Iliwekwa mnamo 2012-09-27.
  3. Microsoft Word - North Test Site _FINAL_.doc (PDF). Iliwekwa mnamo 2012-09-27.
  4. Novaya Zemlya, Northern Russia. NASA. Jalada kutoka ya awali juu ya 2006-10-11. Iliwekwa mnamo 2006-10-14.
  5. Novaya Zemlya in: Encyclopaedia Britannica (11th ed.) (1911). Iliwekwa mnamo 2006-10-14.
  6. 6.0 6.1 Novaya Zemlya in: The Columbia Encyclopedia, 6th ed.. Iliwekwa mnamo 2006-10-14.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Novaya Zemlya travel guide kutoka Wikisafiri

Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Novaya Zemlya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.