Mchanganyiko wa aina moja
Mandhari
Mchanganyiko wa aina moja katika kemia ni mchanganyiko wa dutu mbili au zaidi ambako vijalizo au sehemu zake hazionekani tena pekee. Mfano wa mchanganyiko wa aina moja ni sukari iliyokorogwa katika maji yaani mmumunyo.
Tofauti nao ni mchanganyiko anuwai ambako vijalizo vyake vinaonekana na kutofautishwa kirahisi kwa mfano kiolei cha maji na mafuta, au maji na mchanga.
Kama katika kila mchanganyiko wa kikemia vijalizo haviingii katika muungo kemia kama kampaundi.