Marc Auslander

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Marc Auslander ni mtaalamu wa kompyuta kutoka nchi ya Marekani aliyeshiriki kubuni lugha ya kompyuta "PL/8 compiler". Alitumia maisha yote ya kazi kwenye kituo cha Thomas J. Watson cha kampuni ya IBM kilichoko Yorktown Heights, New York.

Alipokea shahada ya awali ya hisabati kutoka chuo kikuu cha Princeton mwaka 1963. Alijiunga na IBM mwaka huo huo. Mwaka 1991 alitajwa kama IBM-Fellow. Alistaafu mwaka 2004 lakini aliendelea na kujishughulisha na kampuni ya IBM.[1][2]

Auslander alitunga insha za kisayansi 19 akishika hataza 14.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-09-21. Iliwekwa mnamo 2022-07-28. 
  2. "Mr. Marc Auslander". NAE Website. Iliwekwa mnamo 2022-07-28.