Nenda kwa yaliyomo

Mandy (wimbo)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mandy (Toleo la Westlife))
“Mandy”
“Mandy” cover
Single ya Barry Manilow
B-side "Something's Comin' Up"
Imetolewa 1974
Muundo 7" vinyl
Imerekodiwa 1974
Aina Pop
Studio Bell
Mwenendo wa single za Barry Manilow
"Could It Be Magic"
(1973)
"Mandy"
(1974)
"It's a Miracle"
(1975)

"Brandy" ni moja kati ya nyimbo zilizovuma katika mwaka 1971 kutoka kwa watunzi Scott English na Richard Kerr. Ulifanikiwa kufika katika nafasi ya 12 katika chati ya single za Uingereza. Huku toleo la kwanza lilifanya vibaya nchini Marekani. Mwaka 1974 ulirekodiwa na Barry Manilow kama "Mandy". Wimbo huu ulikuwa ni wimbo wa kwanza kutoka kwa mwandishi Manilow kufika katika nafasi ya kwanza katika chati ya Billbord Hot 100 na chati ya Adult Contemporary, na pia ni wimbo wake wa kwanza kupata nishani ya dhahabu.

Wapo waliodhani kuwa, Mwandishi huyu aliandika wimbo huu kwa ajili ya mbwa wake aliyempenda, lakini suala hili limekuwa likitiliwa mashaka. Mwandishi mmoja wa alimpigia simu katika saa za asubuhi na kumuuliza nani hasa aitwa "Brandy" na ndipo bila kutilia maanani alijibu "Mbwa" ili aondokane na kero za mwandishi..[1]

Miaka mitatu baada ya wimbo huu kurekodiwa na Mtunzi wa Kizungu mwaka 1971 na rekodi ya Manilow,aliandika wimbo uliovuma wa "Brandy (You're a Fine Girl)" hii ikiwa ni mwaka 1972. Sasa ili kuondoa mchanganyiko, wakati Manilow alipoamua kutengeneza Wimbo wake aliamua kubadilisha jina la wimbo na kuuita "Mandy". Alikuwa Clive Davis aliependekeza Manilow arekodi wimbo huo. [2] , Mwanzoni Manilow alirekodi wimbo huo katika dizaini ya pop, ambao kidogo ulifanana na wa mwimbaji mwingine, lakini mtengenezaji wake hakupenda staili hiyo, na hivyo Manilow aliamua kurudia kwa mara ya pili katika mahadhi ya taratibu, na ndipo mtengenezaji wake alipoupenda. ulikuwa ni wimbo wa kwanza kutoka kwa Manilow kutengeneza katika studio za Clive Davis' Arista Records chini ya lebo ya (formerly Bell Records) kuweza kufanya vizuri katika chati ya muziki ya Billboard Hot 100. [3]


Wimbo huu, umeshawahi kuimbwa na wanamuziki wengine pamoja na Andy Williams (1975), Richard Clayderman (1994), Johnny Mathis (1997), Me First and the Gimme Gimmes (1997), Bradley Joseph (2005), Raymond Quinn (X Factor runner-up 2006), Donny Osmond (2007).

Toleo la Westlife

[hariri | hariri chanzo]

Wimbo huu pia umeimbwa na kundi la Westlife.Wimbo wa "Mandy" ilikuwa nu single ya pili kutoka katika albamu yao ya Turnaround.

Mtiririko wa nyimbo

[hariri | hariri chanzo]

CD ya kwanza

[hariri | hariri chanzo]
  1. Mandy - 3:19
  2. You See Friends (I See Lovers) - 4:11
  3. Greased Lightning - 3:19
  4. Mandy (Video) - 3:19
  5. Mandy (Making Of The Video) - 2:00

CD ya pili

[hariri | hariri chanzo]
  1. Mandy - 3:19
  2. Flying Without Wings (Live Version) - 3:41
  1. Quoted in The Billboard Book of Number One Adult Contemporary Hits
  2. Allmusic.com
  3. Mandy Songfacts