Malibu's Most Wanted
Malibu's Most Wanted | |
---|---|
Imeongozwa na | John Whitesell |
Imetayarishwa na | Fax Bahr Mike Karz Adam Small |
Imetungwa na | Fax Bahr Adam Small Jamie Kennedy Nick Swardson |
Nyota | Jamie Kennedy Taye Diggs Anthony Anderson Blair Underwood Regina Hall Damien Dante Wayans Jeffrey Tambor Pamoja na Bo Derek Na Ryan O'Neal |
Muziki na | John Debney John Van Tongeren |
Imesambazwa na | Warner Brothers |
Imetolewa tar. | 10 Aprili 2003 |
Ina muda wa dk. | 86 min. |
Lugha | Kiingereza |
Bajeti ya filamu | $15 million |
Mapato yote ya filamu | $34,622,504[1] |
Malibu's Most Wanted ni filamu ya vichekesho ya mwaka wa 2003 ambayo imetungwa na kuchezwa na Jamie Kennedy akiwa na washiriki wenzi Taye Diggs, Anthony Anderson, na Regina Hall.
Filamu hii ilitungwa na waanzilishi wa MADtv, Fax Bahr na Adam Small, ambao pia wamesimama kama watayarishaji wa filamu hii.
Uhusika wa "B-Rad" awali ulionekana kipindi cha kujificha kwenye kamera cha Jamie Kennedy, The Jamie Kennedy Experiment, lakini ilianza tangu enzi zake za ucheshi wake wa wima na kuufanya kama utaratibu endelevu.
Hadithi
[hariri | hariri chanzo]Filamu inaanza katika maisha ya familia ya Bill Gluckman, seneta Myahudi Mzungu kutoka mjini Malibu, California ambaye anagombea Ugavana wa California. Mtoto wake Brad ni Wigger (Wigger ni nadharia ya mtu Mzungu anayefuata tabia au tamaduni za Wamarekani Weusi - hasa katika hip hop), amejipendekeza mwenyewe jina la utani la "B-Rad" licha ya kuwa na utajiri katika familia yake, maisha ya kivulini. Imetokea, wanachama wa Bwana Gluckman wa kampeni za kisiasa wamekuwa na wasiwasi na upuuzi wa Brad, tabia za kishenzi zinazopelekea kuharibu nafasi ya baba'ke asichaguliwe.
Wanachama wa kikosi cha kampeni kimekodisha waigizaji wawili, ambao hawajui undani zaidi wa maisha ya mjini zaidi ya B-Rad, kwa kuigiza kama majambazi, wakamtekanyara, na wakampeleka huko South Central Los Angeles ambapo walitumainia kwamba Brad ataogopa kwa kuwa yeye mzungu - hasa baada ya kushuhudia maisha ya kitaa yapo vipi. Kwa bahati mbaya kila aliyejiingiza, mpango unavurugika baada ya Brad kutaka kujihusisha na vikundi vya kihuni na baadaye akajiingiza mwenyewe na wale waigizaji waliotumwa kuja mzingua nao pia wanamwongoza pabaya.
Washiriki
[hariri | hariri chanzo]Mwigizaji | Uhusika |
---|---|
Jamie Kennedy | Brad "B-Rad G" Gluckman |
Taye Diggs | Sean |
Anthony Anderson | PJ |
Regina Hall | Shondra |
Blair Underwood | Tom Gibbons |
Damien Dante Wayans | Tec |
Ryan O'Neal | Bill Gluckman |
Bo Derek | Bess Gluckman |
Jeffrey Tambor | Dr. Feldman |
Kal Penn | Hadji |
Nick Swardson | Mocha |
Keili Lefkovitz | Monster |
Kellie Martin | Jen |
Greg Grunberg | Brett |
J. P. Manoux | Gary |
Terry Crews | 8 Ball |
Walionekana
[hariri | hariri chanzo]- Snoop Dogg (sauti ya panya)
- Mike Epps (DJ kule klabu)
- Felli Fel
- Hi-C
- Young Dre The Truth
- Drop da Bomb
- Hal Fishman
- Big Boy
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Malibu's Most Wanted katika Internet Movie Database