Majadiliano ya mtumiaji:Yusuph Pius

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jadili dhima ya silabi katika sarufi ya kiswahili

SARUFI YA KISWAHILI[hariri chanzo]

SARUFI YA KISWAHILI Sarufi ni mfumo na kanuni za lugha zinazomwezesha mtumiaji wa lugha kuitumia lugha husika kwa usahihi. Mfumo huo humwezesha mzungumzaji kutunga sentensi zisizo na kikomo ambazo hukubalika na wazawa wa lugha wanaoifahamu lugha hiyo barabara. Hivyo ni dhahiri kwamba kila lugha ya mwanadamu huwa na mpangilio na sheria zinazoilinda ili kuifanya kuwa toshelevu na sanifu, na uzingatiwaji wa kanuni na taratibu hizo kwa mtumiaji humfanya na kumtambulisha kama mmilisi wa lugha hiyo. Sheria za lugha zimegawanyika katika makundi manne yanayojulikana kama matawi ya Sarufi ambayo ni pamoja na; matamshi, maumbo, muundo na maana.

1. SARUFI MATAMSHI Sarufi matamshi ni tawi la sarufi ambalo limejikita katika kuchunguza sauti na matamshi yanayotumika katika lugha Fulani na kulinda matumizi sahihi ya matamshi hayo baina ya watumiaji wa lugha hiyo. Lugha ya Kiswahili kama zilivyokuwa lugha zote duniani ina matamshi ya aina mbili; Irabu na konsonanti. A. Irabu Irabu ni aina ya vitamkwa ambavyo hutolewa pasi na kuwepo kizuizi chochote katika mkondo hewa utokao mapafuni ukipitia katika chemba ya kinywa na chemba ya pua kwenda nje. Lugha ya Kiswahili inazo Irabu tano ambazo ni; /a/, /e/, /i/, /o/, na /u/. B. Konsonanti Konsonanti ni aina ya sauti ambazo hutamkwa kwa kuzuia mkondo hewa kutoka mapafuni, ukipitia chemba ya kinywa na chemba ya pua kwenda nje. Katika lugha ya Kiswahili zipo jumla ya konsonanti zifuatazo; /b/, /ch/, /d/, /dh/, /f/, /g/, /gh/, /h/, /j/, /k/, /l/, /m/, /n/, /ny/, /ng’/, /p/, /r/, /s/, /sh/, /t/, /th/, /v/, /w/, /y/ na /z/.


2. SARUFI MAUMBO. Hili ni tawi la sarufi ambalo hujishughulisha na uchunguzi wa maumbo mbalimbali ya maneno katika lugha ya Kiswahili. Maumbo hayo ni; silabi, mofimu na neno lenyewe.

A. Silabi Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za Lugha hutamkwa mara moja kwa pamoja kama fungu moja la sauti. Kuna aina mbili za silabi, yaani silabi funge na silabi huru. Silabi huru ni zile ambazo huishia na irabu. Kwa mfano; la, ma, kwa, mba, n.k.

Ilhali silabi funge ni zile zinazoishia na konsonanti ambapo katika lugha ya Kiswahili ni nadra kuzipata maana lugha hii inatumia silabi huru lakini hupatikana katika maneno ya Kiswahili yanayokopwa kutoka katika lugha nyingine.

Kwa mfano; Alhamisi – a-l-ha-mi-si Taksi - ta-k-si Miundo ya Irabu za Kiswahili a. Muundo wa irabu peke yake (I) - Yapo maneno katika lugha ya Kiswahili yanayoundwa na irabu peke yake kama silabi. Mfano; u+a = Ua, o+a = Oa, a+u = Au, n.k. b. Muundo wa konsonanti pekee (K) – Kiswahili hakina maneno mengi yanayoundwa na silabi pekee isipokuwa maneno machache ambayo huwa ni ya nazali /M/ na /N/ na huwa zinatumika ama mwanzoni au katikati ya neno. Mfano; m+ke = Mke, m+bwa = Mbwa, n+chi = Nchi n.k c. Muundo wa konsonanti na irabu (KI) – Katika muundo huu konsonanti hutangulia irabu. Mfano; b+a = Ba, k+a = Ka n.k. d. Muundo wa konsonanti mbili na irabu (KKI) – Katika muundo huu konsonanti mbili hutangulia irabu. Mara nyingi konsonanti ya pili huwa ni kiyeyusho. Mfano; k+w+a = Kwa, m+w+a = Mwa, b+w+a = bwa, n+d+e = Nde, n.k. e. Muundo wa konsonanti tatu na irabu (KKKI) – Muundo wa namna hii hujitokeza katika maneno machache. Mfano; Bambwa, Tingwa, Tindwa, Mbwa, n.k. f. Muundo wa silabi funge – Huu hujitokeza katika maneno machache ambayo huwa ya mkopo. Mfano; Il-ha-li = Ilhali, Lab-da = Labda B. Mofimu Mofimu ni kipashio kidogo kabisa cha lugha ambacho kina uwezo wa kusitiri maana ya neno ambalo kwalo limeundwa. AU ni kipashio kidogo kabisa cha lugha chenye maana kisarufi.

AINA ZA MOFIMU Mofimu ni kipashio dhahania cha umbo fulani amabcho kinaweza kuwakilishwa na mofu tofautitofauti katika mazingira anuwai. Mofimu huru ni aina ya mofimu ambayo huweza kusimama pekee na kujitosheleza kimaana yaani huwa na sifa ya neno. Mfano; mama, Baba, Dada, Kaka, Mjomba, Shangazi n.k. Kwa kuangalia utagundua kuwa mofimu huru haziwezi kugawanyika zaidi na kubeba maana kisarufi, kwa maana kwamba mofimu ‘baba’ ikigawanywa ba-ba, ‘ba’ hii haina maana yoyote kisarufi zaidi ya kuwa silabi.

Mofimu tegemezi ni aina ya mofimu ambayo huweza kuvunjwavunjwa na kubeba maana kisarufi, mofimu tegemezi hutegemeana ili kuleta maana kamili ya neno. Mfano; neno ‘anakula’ limeundwa na mofimu zifuatazo:- [a-na-kul-a] ambazo kila moja hubeba dhana Fulani ya kisarufi.

VIAMBISHI Ni mofimu zinazopachikwa nyuma au mbele ya mzizi wa neno ili kubadilisha dhana ya neno. Kwa kuwa mofimu hizo hupachikwa sehemu mbili tofauti, tunapata aina mbili za viambishi kwa mujibu wa nafasi zake katika neno yaani; viambishi awali ambavyo hupachikwa mwanzoni au nyuma ya mzizi wa neno,viambishi kati ambavyo hupachikwa katikati ya neno (Kiswahili hakina viambishi hivi) na viambishi tamati ambavyo hivi hupachikwa mbele au mwishoni mwa mzizi wa neno. Mfano:- VIAMBISHI AWALI MZIZI WA NENO VIAMBISHI TAMATI NENO JIPYA

   A	    na	           chez	     ew	    a	Anachezewa
   Wa	     li	           chez	     ean	    a	Walichezeana
   Tu	    ta	           chez	     e	    a	Tutachezea
 

1. Viambishi awali Hivi hupachikwa kabla ya mzizi wa neno na huwa ni vya aina tisa:- i. Viambisha awali vya nafsi- hivi hudokeza upatanishi wa nafsi katika kitenzi, zipo nafsi tatu, nafsi ya kwanza, ya pili, nay a tatu.

NAFSI UMOJA UWINGI Ya Kwanza Ni- Tu- Ya Pili U- M- Ya Tatu A- Wa-


M


Mfano:- Ninalima Tunacheza

ii. Viambishi awali vya ngeli- hivi hupatikana mwanzoni mwa nomino au vivumishi ili kudokeza hali ya umoja na uwingi.

Mfano:- Mtu (umoja) – Watu (uwingi) Msafi (umoja) – Wasafi (uwingi)

iii. Viambishi awali vya ukanushi - hivi hudokeza hali ya uhasi wa tendo. Huwakilishwa na mofimu (ha-) na (si-)

Mfano:- Amekula (uyakinifu) – Hajala (ukanushi), Nakula (uyakinifu) – Sili (ukanushi) iv. Viambishi awali vya Njeo- hivi hudokeza nyakati mbalimbali ambazo ni wakati uliopita, uliopo na ujao.

NYAKATI MOFIMU Uliopo -Na- Uliopita -li- Ujao -Ta-

Mfano:- Mlituona Utakuja

v. Viambishi awali vya hali- hivi hudokeza hali mbili za nyakati ambazo ni mazoea ambayo huwakilishwa na mofimu {hu} na timilifu inayowakilishwa na mofimu {me}. Mfano:- Hucheza Amelima

vi. Viambishi awali vya masharti- hivi hudokeza hali ya masharti au uwezekano katika tendo. Mofimu hizo ni kama –ki-, nge-, ngali- n.k.

Mfano:- ukija Ungekuja Angalimkuta

vii. Kiambishi cha urejeshi wa mtenda (kiima)- mhiki hudokeza urejeshi wa nomino inayotenda katika kitenzi.

Mfano: - Aliyekuja {-ye-} hudokeza urejeshi wa mtenda.

viii. Kiambishi kiwakilishi cha mtendwa au mtendewa (shamirisho) – hivi huwakilisha mtendwa au mtendewa wa jambo. Mfano; Nilimpiga, Uliukata, Nimeipenda, Wameniteta.

ix. Kiambishi awali cha kujirejea (kujitendea) – hiki huwakilishwa na mofimu (-ji-) Mfano; kujipenda

2. Viambishi tamati – Hivi hudokeza kauli mbalimbali za vitenzi. Mfano: - Anacheza – kutenda Unachezwa- Kutendwa Utachezewa- Kutendewa Nimemlia- Kutendea Wamewasomesha- Kutendesha n.k

Mzizi Kiambishi cha Kauli Kiambishi tamati maana Neno jipya Kauli Viambishi vya kauli Chez a Cheza Kutenda -a e a Chezea kutendea -e- Pig ian a Pigiana Kutendeana -ian-/-ean- iw a Pigiwa Kutendewa -iw-/ew- Som esh a Somesha Kutendesha -ish-/esh- eshw a Someshwa Kutendeshwa -ishw-/eshw- Lim ik a Limika Kutendeka -ik-/-ek- an a Limana Kutendana -an- w a Limwa Kutendwa -w-

DHANA YA MZIZI NA SHINA LA KITENZI

Mzizi wa kitenzi ni sehemu ya neno inayobakia mara baada ya kuondoa viambishi vyote vya awali na tamati katika neno hilo. Mfano: - a-na-chez-a {-chez-}, m-ku-lim-a {-lim-} Mzizi funge ni ule ambao hauwezi kujikamilisha kimaana yaani hauwezi kusimama kama neno. Mfano; -lim-, -chez-, -imb- n.k. Mzizi huru ni ule ambao huweza kusimama kama neno na ukichanganuliwa zaidi hupoteza maana yake ya msingi. Mfano; Kinu, Kazi, Arifu, Sali n.k.


Shina la kitenzi ni sehemu ya neno ambayo huongezwa viambishi fuatishi (tamati) au ni sehemu ya neno ambayo hubakia baada ya kuondolewa viambishi tangulizi. Mfano:- chez+a = cheza, lim+a = lima. Sehemu hii ya neno hutumika kuundia neno jipya. Shina sahili – hili ni shina ambalo huundwa na mofimu moja tu ambayo ni mzizi wa neno hilo, huwa ni mofimu huru, Mfano; Kesho, jana, kitabu, jarida n.k. Shina changamano – shina hili huundwa na mzizi na kiambishi tamati maana. Mfano; cheka, lala, lia, kula n.k Shina ambatani – shina hili huundwa na mofimu mbili ambazo ni huru. Mfano; mwana + kwenda = mwanakwenda, mbwa + mwitu = mbwamwitu


UAMBISHI WA MANENO Uambishi Uambishi ni ule utaratibu wa kuongeza viambishi katika mzizi wa neno, ili kulipa neno maana ya ziada. Kiambishi: Kiambishi ni mofu ambayo huambikwa kwenye mzizi wa neno ili kulipa neno hilo maana ya ziada. Tunapopachika mofu hizo mwanzoni au mwishoni mwa mzizi wa neno, hali hiyo huitwa ‘uambishi’. Uambishi upo wa aina mbili; Uambishaji na Unyumbuaji.


UAMBISHAJI Ni aina ya uambishaji ambao huhusisha kurefusha neno na kuliweka katika hali tofauti za kategoria ileile. Uambishaji wa kategoria mbalimbali za maneno. Uambishaji wa vitenzi – Uambishaji wa vitenzi hujitokeza kwa kutegemea dhima tofauti tofauti za mofimu kama vile:- i. Viambishi vya nafsi ii. Viambishi vya njeo iii. Viambishi vya ukanushi iv. Viambishi vya urejeshi v. Viambishi vya hali vi. Na viambishi vya kujitendea Mfano; mzizi –lim- unaweza kupachikwa viambishi hivyo na kuweza kubadilika kidhana kama ifuatavyo:- A-na-lim-a Hu-lim-a U-me-lim-a Ni-na-vyo-lim-a n.k.

Uambishaji wa majina– Uambishaji wa majina huwa unazingatia upatanisho wa kisarufi kimofolojia ambao hujikita katika kuangalia alomofu tofauti zinazowakilisha ngeli moja katika umoja na uwingi wa majina hayo. Kwa mfano:- UMOJA WINGI ALOMOFU m-tu Wa-tu M/WA m-ti mi-ti M/MI Ki-ti vi-ti KI/VI u-gonjwa Ma-gonjwa U/MA Ø-fisadi Ma-fisadi Ø/MA Ø-kaka Ø-kaka Ø/ Ø

Uambishaji wa Viwakilishi. Mfano; Mimi = miye, Sisi = siye, Ambalo, Ambacho, Ambao, Ambaye n.k. UNYAMBUAJI Ni hali ya kupachika viambishi katika mzizi wa neno na neno hilo kubadilika kategoria. Unyumbuaji mara nyingi huhusisha upachikaji wa mofimu fuatishi. Unyambuaji wa kategoria mbalimbali za maneno ya Kiswahili. i. Majina kuwa kielezi. Mfano: Nyumba+ni = Nyumbani, Shamba+ni = Shambani, Ki+raia = Kiraia, Ki+toto = Kitoto n.k. ii. Vivumishi kuwa vitenzi. Mfano: Safi = Safisha, Refu = Refushan.k. iii. Vivumishi kuwa kielezi, Mfano: Ki+pole = Kipole, Ki+vivu = kivivu n.k iv. Vitenzi kuwa majina. Mfano: Lima-Kulima, Cheza – Mchezo, Lia - Kilio n.k. Ukitazama kwa makini utangundua kwamba unyambulishaji mara nyingi hubadilisha neno kutoka katika kategoria moja na kuipeleka katika kategoria nyingine. DHIMA ZA UNYAMBULISHAJI i. Kuongeza msamiati wa lugha ya Kiswahili. ii. Hupanua maana ya neno.


TABIA ZA VITENZI VYA KISWAHILI Vitenzi vya Kiswahili huwa na tabia tofauti tofauti zinazotokana na dhima za mofimu ambazo hupachikwa katika vitenzi hivyo, hivyo kulingana na dhima za mofimu, vitenzi vya Kiswahili huwa na tabia zifuatazo:- A. Kutambulisha nafsi. Mfano:- Anayesoma B. Kutambulisha tendo. Mfano:- Cheza, Lima, Imba n.k. C. Kutambulisha wakati. Mfano:- Ulikuja D. Kutambulisha hali ya uyakinishi na ukanushi. Mfano:- Anacheka – Hacheki E. Kutambulisha kauli mbalimbali za tendo. Mfano:- cheza-chezwa-chezewa-chezeka n.k. F. Kutambulisha hali ya tendo. Mfano:- Huimba, Amekula. G. Kuonesha urejeshi wa mtenda, mtendwa na mtendewa ambao hujidhihirisha katika ngeli ya nomino iliyotajwa kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi. Urejeshi huo ni wa O-rejeshi. Katika urejeshi huo vitenzi hubeba viambishi ngeli vya –O- isipokuwa kama nomino ni ya ngeli ya kwanza umoja ambapo hutumia –e- badala ya –O-. Mfano:- NGELI KIAMBISHI CHA O- REJESHI MFANO A-WA -YE- na –O- Aliyepiga / Waliokuja U-I -O- na –YO- Uliokatwa / Iliyokatwa LI-YA -LO- na –YO- Lililochanika / Yaliyochanika KI-VI -CHO- na –VYO- Kilichovunjika / Vilivyovunjika I-ZI -YO- na –ZO- Iliyofungwa / Zilizofungwa U-ZI -O- na -ZO Uliokatika / Zilizokatika U-YA -O- na –ZO- Ulionipata / Yaliyonipata KU -KO- Kulikotokea PA-MU-KU PO-MO-KO Pale alipoingia / Mule alimotokea / Kule alikofunga



C. Neno Ni silabi au mkusanyiko wa silabi zinazotamkwa au kuandikwa ambazo huwa na maana (maana yaweza kuwa ni ya kileksika au kisarufi).

AINA ZA MANENO

1. NOMINO Ni aina ya neno ambalo hutaja mtu, kitu, mahali, hali na kitendo. Mfano; Mwajuma, Kalamu, Mwanza, Udakitari, Kulima n.k.

Aina za nomino: • Nomino za pekee: Nomino za pekee hutaja na kutambulisha nomino mahsusi na za kipekee. Yaani kuwa kitu ni hicho na wala si chengine chochote. Hizi ni nomino zinazohusisha majina kama vile ya watu, nchi, miji, mito, milima, maziwa na bahari. Herufi za kwanza za nomono za pekee huwa kubwa hata kama nomino hizi zinapatikana katikati ya sentensi. Mfano; baba, Asha, Tanzania, Dodoma, Kilimanjaro, Victoria n.k

• Nomino za jamii: Hizi kwa jina jengine huitwa nomino za jumla. Nomino hizi hazibainishi wazi wazi vitu ambavyo habari zake zinatolewa. Kwa mfano ikiwa ni mtu, mahsusi hatambuliwi. Haituambii kama ni Kelvin, Tuafu ama Zawadi.Ikiwa ni ziwa halitambuliwi kama ni Michigan , Victoria au Nyasa, yaani hutaja vitu bila kutaja umahsusi wake kama ilivyo katika nomino za pekee. Hizi zinapoandikwa si lazima zianze kwa herufi kubwa isipokuwa zimetumiwa mwanzoni mwa sentensi au zimetumika kama anuani ya kutajia kitu kama vile Mkuu wa Sheria. Katika mfano huu ‘sheria’ kwa kawaida ni nomino ya kawaida, lakini hapa inaanza kwa herufi kubwa kwani inataja anuwani ya kipekee. Mfano wa nomino za kawaida ni; Mwanafunzi, Mwalimu, Mnyama, Mtazamaji, Askari n.k

• Nomino za kawaida: Kundi hili la nomino hutumia kigezo cha uwezekano wa kuhesabika kuziainisha. Hapa tunatofautisha kati ya nomino zinazowakilisha vitu vinavyohesabika kwa upande mmoja, na vile visivyohesabika kwa upande mwengine. Nomino ya vitu vinavyohesabika vitanda, nyumba, vikombe vitabu kadahlika. Zile zisizohesabika hurejelea vitu ambavyo hutokea kwa wingi na haviwezi kugawika, kwa mfano maji, mate, makamasi, maziwa, moshi, mafuta. Aghlabu nomino hizo huwa sawa katika umoja na wingi.

• Nomino za kitenzi jina: Hizi ni nomino zinazohusu vitenzi . Huundwa kwa kuongezwa kiambishi {ku-} cha unominishaji kwenye mzizi wa kitenzi cha kitendo halisi ili kukifanya kiwe nomino. Mfano; Kulima, Kucheza, Kuimba n.k

• Nomino dhahania: Hizi ni nomino ambazo hurejelea vitu vinavyoweza kuhusika na mwanaadamu kupitia milango ya hisia kama macho, mapua, masikio vidole na ulimi- yaani vitu ambavyo haviwezi kushikika, kuonekana, na kuonjeka. Mfano; Vita, Njaa, Ugonjwa, Shetani, Mungu n.k

2. VIVUMISHI • Ni maneno ambayo hutoa ufafanuzi au maelezo ya ziada kuhusu jina ili kuitambulisha vyema.

          Aina za vivumishi.

• Vivumishi vya sifa: hutoa sifa za nomino /kiwakilishi cha nomino. Sifa hizi huweza kuwa nzuri, mbaya au yoyote ile. Mfano; mzuri, mbaya, mrembo n.k • Vivumishi vya idadi: vinaweza kujitokeza katika aina tatu ndogondogo. Vivumishi vya aina hii hutoa taarifa kuhusu idadi ya nomino ambazo kiwango chake kimetajwa. Mfano; wawili, watano, wengi, wachache n.k• • Vivumishi vya kumiliki: Ni vivumishi vinavyoonesha kuwa kitu fulani kina milikiwa na mtu au kitu chengine. Mfano; yangu, yake, yako, kwetu n.k • Vivumishi Vioneshi: Vivumishi vya aina hii huonyesha mahali au upande kitu kilipo. Vivumishi vya aina hii hujengwa na mzizi {h} kwa vitu vilivyopo karibu na mzizi {le} kwa vitu vilivyo mbali. Mfano; hapa, pale n.k • Vivumishi vya kuuliza: Hivi ni vivumishi ambavyo hufafanua nomino kwa kuuliza habari zake. Hujibu swali “gani? ipi? ngapi?” • Vivumishi vya pekee: Vivumishi hivi huitwa vya pekee kwa sababu kila kimojawapo huwa na maana maalumu. Pia kila kimojawapo huchukua upatanisho wake wa kisarufi kulingana na ngeli ya nomino ambayo kinaivumisha. Mizizi vivumishi hivi ni ote, o-ote, enye, -enyewe, - ingine, -ingineo. –ote. Huonyesha ujumla wa kitu au vitu -o-ote Kivumishi cha aina hii kina maana ya “kila”, “bila kubagua” – enye Kivumishi cha aina hii hutumika kuleta dhanna ya umilikishaji nomino Fulani. – enyewe Kivumishi cha aina hii hutumika kuisisitiza nomino fulani. – ingine Kivumishi cha aina hii huonyesha/huonesha ‘tofauti na’ au ‘zaidi ya’ kitu Fulani. – ingineo Kivumishi cha aina hii hutumika kuonesha/kuonyesha ziadi. • Vivumishi vya A- unganifu: Vivumishi vya aina hii huundwa kwa mzizi wa kihusishi a- unganifu. Kihusishi hiki huandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho huvumisha nomino iliyotajwa awali. Vivumishi vya aina hii hutumika kuleta dhanna zifuatazo:- -Umilikaji -Nafasi katika orodha. Mfano; wa kwangu, wa Juma, ya tano ya Sita n.k

4. VIELEZI Maana ya vielezi: Vielezi ni maneno yanayofafanua vitenzi, vivumishi au vielezi vyengine. Huweza kuarifu kitendo kilichotendeka kilitendeka wapi , namna gani na hata mara ngapi?

Aina za vielezi • Vielezi vya namna au jinsi. Vielezi vya namna hii huonyesha jinsi au namna kitendo kilivyotendeka. Vielezi vya namna vipo vya aina kadhaa. - Vielezi vya namna halisi. Hivi ni vielezi vinavyotumia maneno ambayo kimsingi yana sura ya vielezi moja kwa moja katika uainishaji wa aina za maneno. Mfano; kuimba sana -Vielezi vya namna mfanano Hivi ni vielezi ambavyo hutumika kufananisha vitendo na vivumishi au nomino mbalimbali. Hujengwa kwa kuongeza kiambishi (ki-) au kiambishi (vi-). Viambishi hivi hujulikana kwa jina la viambishi vya mfanano. Ulifanya vizuri kumsaidia mwanangu.


-Vielezi vya namna vikariri Hivi ni vielezi ambavyo hufafanua vitenzi kwa kurudiarudia neno moja mara mbili. Mfano; polepole, harakaharaka. - Vielezi vya namna hali Hivi ni vielezi ambavyo hufafanua juu ya kitendo kilichotendeka kimetendeka katika hali gani. Mfano; kivivu, kibabe, kizembe, kipole n.k - Vielezi vya namna ala/kitumizi Hivi ni vielezi vinavyotaja vitu ambavyo hutumika kutendea kitendo. Mfano; kwa kisu, kwa kalamu n.k - Vielezi vya namna viigizi. Hivi vinaelezea zaidi jinsi tendo lilivyofanyika kwa kuigiza au kufuatisha sauti inayojitokeza wakati tendo linapofanyika au kutokea. Mfano; alimpiga paaaah! • Vielezi vya idadi. Vielezi vya namna hii huonyesha kuwa kitendo kilitendeka mara fulani au kwa kiasi fulani. Mfano; amempiga mara mbili • Vielezi vya mahali.. Vielezi vya namna hii huonyesha mahali ambapo kitendo kinatokea.Huweza kudokezwa kwa viambishi au kwa maneno kamili. Mfano; amekaa jikoni • Vielezi vya wakati: Vielezi vya namna hii huonyesha wakati wa kutendeka kwa kitendo.Huweza kutokea kama maneno kamili au hodokezwa kwa kiambishi {po.} Mfano; alimkaribisha alipokuja.

5. VITENZI Kitenzi ni neno linaloeleza jambo lililotendwa au lililotendeka. Kitenzi huarifu lililofanyika au lililofanywa na kiumbe hai chochote kinachoweza kutenda jambo. Kitenzi cha Kiswahili huundwa na mzizi pamoja na viambishi vyenye uamilifu wa aina tofauti.

AINA ZA VITENZI • Vitenzi vikuu (T): Vitenzi vikuu ni vile ambavyo hubeba ujumbe muhimu wa kiarifu cha sentensi. Mfano; Mtoto amekuja.

• Vitenzi visaidizi: Hivi hutoa taarifa ya kusaidia vitenzi vikuu. Hutoa taarifa kama vile uwezekano , wakati, hali n.k.Vitenzi visaidizi daima hutumika na vitenzi vikuu, ndivyo vinavyobeba viambishi vya wakati. Mfano; Alikua anacheza, Huwa namfurahia.  Vitenzi visaidizi huweza kupachikwa urejeshi wa nomino na kusaidia kuifafanua nomino hiyo. Mfano; motto aliyekua anacheza. Virejeshi hivyo ni kama; -ye-, -yo-, -o-, -lo-, -cho-, -wo- n.k

• Vitenzi vishirikishi: Hivi ni Vitenzi ambavyo hufanya kazi ya kuunga sehemu mbili za sentensi. Havichukui viambishi vya nafsi, njeo ama hali. Vitenzi vishirikishi ni vya aina mbili, ambavyo ni kitenzi kishirikishi “ni” cha uyakinishi na kitenzi shirikishi “si” cha ukanushi. Kazi za kitenzi kishirikishi -kushirikisha vipashio vingine katika sentensi -Kuonesha tabia fulani iliyopo au isiyokuwepo ya mtu fulani au kitu fulani. -Kuonyesha cheo au kazi anayofanya mtu. -kuonyesha sifa za mtu. - kuonyesha umoja wa vitu au watu -kuonyesha mahali -kuonyesha umilikishi wa kitu chochote. 6. KIWAKILISHI Kiwakilishi ni aina ya neno linaloweza kutumika badala ya jina .

AINA ZA VIWAKILISHI • Viwakilishi vya kuuliza/viwakilishi viulizi ambavyo huashiriwa na mofu / kiambishi {-pi} ambavyo katika tungo hutanguliwa na kiambishi ngeli cha jina husika. Mfano- Mtoto yupi • Wiwakilishi vya urejeshi ambavyo vinajengwa na shina amba pamoja na vipande vidogo vidogo –ye-, -o-, -cho-, vyo, lo, po, mo, ko n.k ambavyo vinachaguliwa kilingana na ngeli ya majina yanayorejeshwa navyo. • Viwakilishi vya idadi: Viwakilishi hivi hutuarifu kuhusu idadi ya nomino hiyo huweza kuwa kamili (halisi) au ya jumla. Mfano; Wengi wamekuja • Viwakilishi vya pekee:- Hivi ni aina ya vivumishi vya pekee kuwakilisha nomino. Hufuata sheria za upatanisho za nomino zinazowakilishwa. • Viwakilishi vya A-unganifu:- Viwakilishi hivi huundwa kwa kihisishi cha A-unganifu kusimamia nomino iliyomilkiwa, inayochukuwa nafasi fulani katika orodha au nomino ya aina fulani. Kihisishi a-unganifu huandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho husimama mahali pa nomino.

7. VIUNGANISHI Ni maneno, kikundi cha maneno au kiambishi chenye kuunganisha maneno, kirai, kishazi au sentensi.Dhima ya kiunganishi ni kuunga vipashio viwili au zaidi vyenye hadhi sawa kisarufi.

Aina za viunganishi: • Viunganishi huru: hivi ni viunganishi vinavyosimama pekee katika tungo, katikati ya vipashio vinavyo ungwa. Hujumuisha: - -Viunganishi nyongeza/vya kuongeza. Mfano; Tena, Na, Zaidi ya n.k. - Viunganishi vya sababu/visababishi. Mfano; Kwa kuwa, kwa sababu kwa vile, kutokana na, n.k. - Viunganishi linganishi/vya kinyume. Mfano; Ingawa, Japokuwa, Lakini n.k. - Viunganishi vya wakati. Mfano; kasha, baadaye, Halafu, Baada ya n.k. - Viunganishi vya masharti. Mfano; Kama, Ikiwa, Iwapo n.k - Viunganishi vihusishi Mfano; Cha, La, Wa, Za n.k.

• Viunganishi tegemezi: Ni viambishi ambavyo hutiwa katika kitenzi cha kishazi tegemezi ili kukiunga na kitenzi kikuu cha kishazi huru ambavyo kwa pamoja huunda sentensi changamano au shurtia. Mfano; -ye-, -po-, -ki-, -cho- na -nge-.


8. VIHUSISHI Ni maneno ambayo huonyesha uhusiano uliopo baina ya neno moja na jengine. Vihusishi aghlabu huonyesha uhusiano kati ya nomino au kirai nomino na maneno mengine. Mambo mbalimbali yanayoweza kuonyeshwa na vihusishi - huonyesha uhusiano wa kiwakati - huonyesha uhusiano wa mahali - huonyesha uhusiano wa kulinganisha - huonyesha uhusiano wa umilikaji - huonyesha uhusiano wa sababu/kiini

Aina za vihusishi

-vihusishi vya wakati Mfano; kabla ya, baada ya n.k -vihusishi vya mahali Mfano; chini ya, juu ya, ndani ya, mbele ya n.k. - vihusishi vya ulinganishi/ vya kulinganisha Mfano; kuliko, zaidi ya n.k. -vihusishi vya sababu/ kusudi/nia Mfano; kwa sababu ya, kwa ajili ya n.k. -vihusishi vya ala (kifaa)- Mfano; kwa - vihusishi vimilikishi Mfano; cha, za n.k. -vihusishi vya namna/jinsi/hali Mfano; moto wa kuotea mbali, macho ya mviringo Matumizi ya ziada ya kihusishi “kwa” -kihusishi hiki huonyesha mahali au upande -kihusishi hiki huonyesha sababu au kisababishi cha jambo -kihusishi hiki huonyesha wakati -kihusishi hiki huonyesha sehemu Fulani ya kitu kikubwa -kihusishi hiki hutumika kuonyesha ‘nia ya pamoja na’ -Kihusishi hiki huonyesha jinsi kitendo kilivyotendeka

9. VIHISISHI / VIINGIZI Ni maneno ambayo hudokeza hisia za moyoni mwa mzungumzaji baada ya kuwa katika hali ya furaha, huzuni, majonzi, maumivu, kushangaa, majuto n.k. Mara tunapotumia viingizi katika tungo huathiri tungo hiyo kuifanya kuwa na mshangao, hivyo tunaongeza alama ya mshangao mbele ya tungo hiyo. Kwa kuzingatia hisia tunaweza kuwa na aina ya viingizi zifuatazo:- • Viingizi vya huzuni – pole! Jamani! Maskini! N.k • Viingizi vya mshangao – waow! Lahaula! Eboo! Haiii! Ati! • Viingizi vya kuitika – abee! Lamaa! Naam! • Viingizi vya kutakia heri – Inshallah! • Viingizi vya kiapo – Wallah! Haki ya nani! Kweli kabisa!














3. SARUFI MUUNDO Sarufi muundo hujihusisha na kushughulikia mpangilio na mfuatano wa maneno katika tungo ili yaweze kujitosheleza kimaana. Katika sarufi muundo tunaangalia mijengo ya tungo za kiswahiali.

TUNGO Tungo ni huwa ni matokeo ya kuviweka pamoja vipashio sahili vya lugha ili kujengana hata kipashio kikubwa kabisa cha lugha. Tungo ina asili yake katika mzizi ‘Tunga’ ukiwa na maana ya kuibua kitu kipya kabisa au kushikamanisha vitu pamoja ili kupata ‘utungo’. Tungo hujidhihirisha katika viwango vine ambavyo hutupatia vipashio vya tungo:-  Kiwango cha neno ambacho hujengwa na mofimu  Kiwango cha kirai ambacho hujengwa na neno  Kiwango cha kishazi ambacho hujengwa na kirai  Kiwango cha sentensi ambacho hujengwa na kirai au kishazi

1. NENO Ni silabi au mkusanyiko wa silabi zinazotamkwa na kuandikwa na kuleta maana katika lugha husika. Neno huundwa na mofimu. Ikiwa ni mofimu huru neno huwa neno huru lakini neno likiundwa na mofimu tegemezi neno huwa changamano. Zipo aina nane za maneno katika lugha ya Kiswahili ambazo ni:- i. Nomino ii. Kivumishi iii. Kiwakilishi iv. Kitenzi v. Kielezi vi. Kiunganishi vii. Kihisishi na viii. Kihusishi. (rejelea aina za maneno kwa ufafanuzi zaidi)


2. KIRAI Ni kipashio cha lugha ambacho huwa na muundo wa neno moja au zaidi lakini huwa hakina muundo wa kiima na kiarifu. Muundo wa kirai huwa ni wa neno moja au zaidi ambayo huwa pamoja katika mpangilio maalumu wenye kuzingatia uhusiano wa maneno hayo na neno kuu ambalo ndio huwa linabeba aina ya kundi hilo la maneno. AINA ZA VIRAI A. Kirai nomino (KN) Hili ni kundi la maneno ambalo hutawaliwa na nomino. Kirai nomino huundwa na maneno yafuatayo:- o Nomino pekee. Mfano; Asha anapika, Nyangoye anaimba, Nyegera anacheza (N) o Nomino mbili au zaidi zinazounganishwa. Mfano; Mhindi na Sagati wanacheza. (N+U+N) o Nomino na kivumishi. Mfano; Mtoto mnene amekuja, Mzee mfupi ameondoka. (N+V) o Kiwakilishi pekee. Mfano; Yule ameondoka, Wewe umenena, Wale waliokuja. (W) o Kiwakilishi na kivumishi. Mfano; Yule mvivu amerudi, Wewe mlemavu njoo. (W+V) o Nomino na kitenzi jina. Mfano; Mchezo wa kusisimua, Wimbo wa kupendeza. (N+Ktj) o Nomino na kishazi tegemezi kivumishi. Mfano; Mjukuu aliyepotea, Mheshimiwa aliyeondoka. (N+βV) B. Kirai kivumishi (KV) Hiki ni kirai ambacho muundo wake umejikita katika kivumishi na maneno yanayohusiana na kivumishi katika tungo tungo hiyo. Virai hivi kwa kawaida hujibainisha zaidi kimuundo kama sehemu ya virai nomino. Virai hivi huundwa na:- o Kivumishi na Kirai nomino. Mfano; Mwenye mali nyingi, Wenye watoto wengi. o Kivumishi na kielezi. Mfano; Mzuri sana, Mweupe pee!, Mweusi tii!, Mbaya sana. o Kivumishi na kirai kitenzi. Mfano; Mwenye kupiga gitaa, Mwenye kupenda sana. o Kivumishi na kirai kiunganishi. Mfano; Nzuri ya kupendeza, Mpungufu wa akili. C. Kirai kitenzi (KT) Ni kirai ambacho kimekitwa katika kitenzi, au katika uhusiano wa kitenzi na neno au mafungu ya mengine ya maneno. Hii ina maana kwamba, neno kuu katika kirai hiki ni kitenzi. Kirai kitenzi kimeundwa na vipashio vifuatavyo:-

o Kitenzi pekee. Mfano; amekuja, amekula, ameoga. (T) o Kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu. Mfano; Alikua anacheza (Ts+T), Alikua anaweza kuimba. (Ts+Ts+T) o Kitenzi kishirikishi na shamirisho. Mfano; Ni mtanashati, Ndiye mwizi, Sio mwelewa. (t+sh) o Kitenzi, jina na kielezi. Mfano; Nimepika uji asubuhi D. Kirai kielezi Tofauti na aina nyingine ya virai, miundo ya virai vielezi haielekei kukitwa kwenye mahusiano ya lazima baina ya neno kuu (yaani kielezi ) na neno au fungu la maneno linaloandamana nalo. Badala yake miuundo inayohusika hapa ni ya maneno ambayo hufanya kazi pamoja katika Lugha kama misemo, neno au maneno yanayofuata neno lililotangulia yakifafanua zaidi neno hilo. Zaidi kirai kielezi huelezea namna, wakati, mahali na kinachofanya tendo hilo litendeke. Mfano; Mara nyingi, Sana sana, Polepole, Jana asubuhi, Kesho mchana, n.k. E. Kirai kihusishi Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika mahusiano baina ya vihusishi kwa, na, katika, au kwenye na fungu la maneno linaloandamana nacho. Kwa maneno mengine kirai hicho ni kile ambacho neno kuu ni kihusishi. Virai vihusishi japokuwa muundo wake hufanana ila hutofautiana kimaana, zipo maana tatuambazo ni:- a) Pahala – kwa baba, katika kabati, kwenye lindo b) Utumizi – Kwa kisu, Kwa mkono c) Uhusika – Na Mjomba, Na Bibi.

VIAMBISHI TAMATI MAANA VYA KISWAHILI[hariri chanzo]

Viambishi tamati– Hivi hudokeza kauli mbalimbali za vitenzi. Mfano: - Anacheza – kutenda Unachezwa- Kutendwa Utachezewa- Kutendewa Nimemlia- Kutendea Wamewasomesha- Kutendesha n.k

Mzizi Kiambishi Kiambishi tamati maana Neno jipya Kauli Viambishi vya kauli Chez a Cheza Kutenda -a e a Chezea kutendea -e- / -i- Pig ian a Pigiana Kutendeana -ian-/-ean- iw a Pigiwa Kutendewa -iw-/ew- Som esh a Somesha Kutendesha -ish-/esh- eshw a Someshwa Kutendeshwa -ishw-/eshw- Lim ik a Limika Kutendeka -ik-/-ek- an a Limana Kutendana -an- w a Limwa Kutendwa -w-

Viambishi tamati katika vitenzi vya Kiswahili.

Viambishi tamati katika lugha ya Kiswahili hujitokeza kudokeza dhima kubwa mbili:- I. Viambishi tamati vya kauli II. Viambishi tamati maana

Kiambishi tamati maana – Hii ni mofimu ya mwisho kabisa katika kitenzi yenye dhima ya kukamilisha maana kusudiwa na msemaji wa tungo hiyo. Mfano:- Pig-a, Chez-w-a, Som-esh-a n.k. Mofimu hizi hujitokieza mbele ya viambishi vya kauli au mbele ya mzizi wa neno lenyewe.

Aina za viambishi tamati maana. Viambishi tamati maana vinajitokeza katika aina tofauti mbili ambazo ni; Viasili na Vijenzi.

1. Viambishi tamati maana viasili Hivi ni vile vinavyojitokeza katika shina asilia la kitenzi husika. Viambishi hivi vipo katika makundi mawili:- a) Vyenye asili katika lugha Kiswahili, hivi huwa ni mofimu (-a) Mfano; Pig-a, Chez-a, Omb-a n.k b) Vyenye asili katika lugha za Kigeni, hivi huwa ni mofimu (-i), na (-u) Mfano; Sal-i, Shukur-u n.k.

2. Viambishi tamati maana vijenzi Hivi ni vile ambavyo hujitokeza katika vitenzi vilivyonyambulishwa. Viambishi hivi hujitokeza kukamilisha dhima zifuatazo:- a) Viambishi tamati maana vikanushi, hivi hukamilisha maana iliyokusudia kuonesha ukanushi wa tendo, huwa ni mofimu (-i) Mfano; Sichez-i, Huimb-i, Hawasom-i, Silal-i N.k b) Viambishi tamati maana Vielekezi, hivi hukamilisha maana iliyokusudia kuelekeza jambo, kitenzi hicho huwa na mofimu ya masharti Ka- na mofimu elekezi huwa ni mofimu (-e) Mfano; Kachez-e, Kasom-e, Kalim-e, Kaog-e N.k c) Viambishi tamati maana Vinominishi, hivi ni vile vinavyobadili kitenzi kuwa nomino, huwa ni mofimu (-aji), (-zi), (-shi), (-o) Mfano; Mchez-aji, Mwi-zi, Mche-shi, Pig-o N.k

SARUFI MATAMSHI (FONOLOJIA)[hariri chanzo]

Fonolojia ni nini? Ni tawi la sarufi linalojishughulisha na uchunguzi, uchanganuzi na uanishaji wa sauti pambanuzi za lugha . Kwa maelezo mengine, fonolojia hujihusisha na utaratibu wa mpangilio wa vitamkwa katika maneno ya lugha. Fonolojia kwa upana wake pia hujishughulisha na vipengele kama: matamshi, kiimbo, mkazo, lafudhi, toni, mfuatano wa sauti katika kuunda mofimu, mfuatano katika kuunda neon na otografia.

SAUTI ZA LUGHA YA KISWAHILI 1. Irabu – Ni sauti zinazotamkwa ilhali mkondo wa hewa utokao mapafuni kwenda nje kupitia chemba ya kinywa na pua ukiwa umeachwa wazi bila kuzibwa. Irabu za Kiswahili zipo tano ambazo ni a, e, i, o na u. Sifa bainifu za irabu  Irabu huweza kutofautishwa na kuanishwa kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo: a. Mwinuko wa ulimi, irabu za juu, kati au chini

b. Sehemu ya ulimi ya kutamkia yawezekana ni mbele, kati au nyuma

c. Mkao wa mdomo, mdomo unaweza kuwatandaza au mviringo. Rejea kielelezo hiki:

Hivyo basi, /u/ Ni irabu juu nyuma tandaza /i/ Ni irabu juu mbele siyo tandaza /o/ Ni irabu kati nyuma tandaza /e/ Ni irabu kati mbele siyo tandaza /a/ Ni irabu chini siyo tandaza Kadhalika tunatumia alama // kumaanisha kuwa inayooneshwa ni sauti / foni. 2. Konsonanti – Ni sauti zinazotamkwa kwa kuzuia mkondo wa hewa katika sehemu mbalimbali kinywa ni hasa kwa kutumia ulimi. Sifa bainifu za konsonanti  Konsonanti huweza kubainishwa kwa kuzingatia sifa zifuatazo; a. Mahala pa kutamkia b. Namna ya utamkaji c. Mtetemo wa sauti, ghuna nyuzi za sauti hutetema, si ghuna nyuzi za sauti hazitetemi Jedwali lifuatalo linaonyesha aina za konsonanti kulingana na mahali zinapotamkiwa na sauti (ghuna au sighuna)

Midomo Midomo + Meno Meno + Ulimi Ufizi Kaakaa + ufizi Kaakaa gumu Kaakaa Laini Koo Aina ya Sauti Vipasuo /p/ /b/ /t/ /d/ /j/ /k/ /g/ + - Vikwamizo /f/ /v/ /th//dh/ /s/ /z/ /sh/ /kh//gh/ /h/ + - Vipasuo kwamizo /ch/ + - Nasali/ving’ong’o /m/ /n/ /ny/ /ng’/ + - Vitambaza /l/ + - Kimadende /r/ + - Kiyeyusho/Nusu irabu /y/ /w/ + -