Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano ya mtumiaji:Mzeegabriel

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

WAJIKI TANZANIA

[hariri chanzo]
Faili:WAJIKI Tanzania logo.png
Wanawake katika Jitihada za Kimaendeleo

Wanawake katika Jitihada za Kimaendeleo

[hariri chanzo]

WAJIKI[1], ni shirika lisilo la kiserikali lililosajiliwa kwa lengo la kufanya utetezi wa haki za binadamu, na limejikita zaidi katika utetezi wa haki za wanawake, watoto na makundi maalum.

Shirika linapatikana kata ya Makumbusho, wilaya ya Kinondoni[2], mkoani Dar es Salaam [3].

Lilianzishwa 2009 na kisha kusajiliwa kama shirika lisilo la kiserikali mwezi Juni 23, 2014 ikiwa lengo ni kutokomeza umaskini na ukatili uliokithiri.

Pia shirika lipo katika mitandao mbalimbali ikiwepo mtandao wa wanawake, katiba, uchaguzi na uongozi, mtandao wa mashirika yanayopinga ukatili wa kijinsia (MKUKI), mtandao wa mashirika yanayopinga rushwa ya ngono, mtandao wa mashirika ya utetezi wa haki za watoto na mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika wilaya ya kinondoni.

WAJIKI[4], inafanya shughuli zake za utetezi kwa mbinu mbalimbali kama vile kutoa elimu kupitia semina na warsha mbalimbali na kuendesha kampeni mbalimbali ambapo kwa sasa inaendesha kampeni ya safari salama bila rushwa ya ngono kwa wasichana na wanafunzi inawezekana kwa lengo la kujenga uelewa mpana juu ya ukatili wa rushwa ya ngono.

Matembezi ya kampeni "Vunja Ukimya! Safari Salama bila rushwa ya ngono kwa wasichana na wanafunzi inawezekana"

Shughuli za WAJIKI Tanzania

[hariri chanzo]
  • Utoaji wa elimu juu ya utetezi wa haki za wanawake, watoto na makundi maalumu.
  • Kuanzisha vilabu vya watoto vya jinsia, uongozi na mapambano ya rushwa ya ngono shuleni na mitaani ili kuwa jengea uwezo watoto.
  • Kuendesha kampeni mbalimbali kama vile kampeni ya safari salama bila rushwa ya ngono kwa wasichana na wanafunzi inawezekana, kwa kufanya matembezi ya uhamasishaji, warsha semina na makongamano mbalimbali.
  • Kupinga aina zote za ukatili wa kijinsia na rushwa ya ngono kwa kushirikiana na jamii kuibua matukio ya ukatili wa kijinsia na watoto ikiwemo rushwa ya ngono na kufanya rufaa sindikizi hospitali - polisi - mpaka mahakamani.
  • Kutoa ushauri na usuluhishi kwa migogoro ya kijamii kama vile migogoro ya ndoa na utekelezaji watoto.
  • Kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya afya ikiwepo haki ya afya ya uzazi, kupambana na magonjwa ambukizi, kutoa ushauri nasaha kwa wagonjwa ambukizina utunzaji mazingira.
  • Uwezeshaji wanawake, wasichana na vijana kiuchumi na kijamii kupitia semina warsha mbalimbali.

Red Bull Neymar Jr's Five TZ

[hariri chanzo]
Faili:Red Bull Neymar Jr's Five Logo.png
Red Bull Neymar Jr's Five Tanzania

Red Bull Neymar Jr's Five Tanzania

[hariri chanzo]

Red Bull Neymar Jr's Five ni mashindano ya kimataifa ya mpira wa wachezaji watano kwa watano, yanayoleta wachezaji kutoka kila pembe ya dunia, huku timu zikishindana kote ulimwenguni kufuzu fainali ya kitaifa kuelekea fainali ya dunia kusaka zawadi ya mwisho ya kuiwakilisha nchi yao kwenye fainali ya dunia na kupata fursa ya kuukutana na Neymar Jr.

Ni dhana ya kipekee ambapo kila timu inajaribu "kuwashinda wapinzani wao" nje ya uwanja - kila wakati bao linapofungwa, timu pinzani inapoteza mchezaji. Mshindi wa mechi ni timu ambayo imewatoa wachezaji wote wa timu pinzani nje ya uwanja au timu iliyofunga mabao mengi zaidi hadi mwisho wa mchezo.

Mashindano ya Red Bull Neymar Jr's Tanzania

[hariri chanzo]

Tutakuwa tukiendesha na kusimamia mashindano kwa wanaume na wanawake. Mashindano hayo yatakuwa kwa ngazi ya Taifa, Mikoa na Wilaya. Mashindano ya wanaume na wanawake yatajumuisha timu 32 kwa Taifa, timu 16 kwa Mkoa na timu 8 kwa Wilaya. Mashindano yatafanyika kwa njia ya makundi au ligi kwa kuanzia kwa njia ya awali ya mtoano ili kupata idadi kamili ya timu zinazohitajika kwenye kila ngazi.

Muhtsari wa sheria za Red Bull Neymar Jr's Five

[hariri chanzo]
  • Kila timu inaweza kusajili wachezaji wasiozidi 7 (Wachezaji 5 + 2 Akiba)
  • Kila timu itakuwa na viongozi watatu tu katika safu ya uongozi ambao ni Meneja, Kocha na Mjumbe mmoja wenye kufanya jukumu lolote la timu.
  • Mchezo unachezwa kwa mtindo wa 5 v 5 bila golikipa.
  • Kwa kila bao linalofungwa, timu pinzani inapoteza mchezaji mmoja, hivyo, mshindi ni timu ambayo imewatoa wote wachezaji wa wapinzani wao nje ya uwanja au timu iliyofunga mabao mengi zaidi hadi mwisho wa mchezo.
  • Kila mchezo huchukua dakika 10 au hadi timu pinzani isiwe na wachezaji yaani wote wametolewe.

Washiriki wa shindano la Red Bull Neymar Jr's Five Tanzania

[hariri chanzo]

Washiriki wa shindano wanaweza kushiriki katika mchujo wa kufuzu kitaifa Red Bull Neymar Jr's Five Tanzania kwa wenye umri wa kati ya miaka 16 - 35 na ni wakazi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanaweza kuwa wanafunzi au si wanafunzi, wanachuo au si wanachuo, vilabu vya michezo mbalimbali, Taasisi / makampuni, wakazi n.k.

  1. Wanawake katika Jitihada za Kimaendeleo
  2. [[https://sw.m.wikipedia.org › wiki Wilaya ya Kinondoni - Wikipedia, kamusi elezo huru]]
  3. [[https://en.m.wikipedia.org › wiki Dar es Salaam - Wikipedia]]
  4. Wanawake katika Jitihada za Kimaendeleo