Majadiliano ya mtumiaji:Maziwa Makuu SMM

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

SABABU KWA NINI UTUMIE MITANDAO YA KIJAMII KUTANGAZA BIASHARA NA SHUGHULI ZAKO:

Kabla ya kukua kwa matumizi ya Intaneti, Biashara na Shughuli nyingi zilitumia mbinu ya moja kwa moja( offline marketing tactics) kujitangaza. Kadri matumizi ya Mtandao wa Intaneti yalivyoongezeka kila mtu mwenye biashara na shughuli inayotakiwa kujulikana kwa watu alianza na kuendelea kutumia ili kuwafikia Wateja kwa Urahisi na kwa haraka sana.

Tumeona Makampuni Makubwa kwa Madogo na Taasisi mbalimbali zikifungua wovuti binafsi kuwakirisha shughuli zao. Wovuti hizi zilianzishwa kiutaalamu zikisimama juu kwenye Injini za Utafutaji ( Search Engines) na Maneno Muafaka ( specific keywords). Mfano,Daktari Bingwa wa Meno, kwenye Mtaa wa Gogo, Kariakoo angeanzisha wovuti wenye Maneno Muafaka na Maalum (specific keywords) ‘’Daktari Bingwa wa Meno, Mtaa wa Gogo ,Kariakoo’’ na kujaribu kupata webusaiti nyingine kutuma linki kweye saiti yake kusudi Injini za Utafutaji kama Google ziletee matokeo endapo anayetembelea mtandao wa intaneti angeandika maneno, Daktari Bingwa wa Meno, Mtaa wa Gogo Kariakoo kwa ajili ya kutafuta. Hii inajulikana kitaalamu kama ‘’SEO’’ au ‘’Search Engine Optimization.’’ 

Kutafuta wovuti wa biashara Fulani ilikuwa haitoshi kwa watembeleaji wa mtandao (online searchers), ambao walitaka sio tu kumtafuta Daktari Bingwa wa Meno, Mtaa wa Gogo, Kariakoo, lakini kutaka kusikia pia wengine wanasema nini kuhusu Daktari huyo! Kutokana na mahitaji hayo kukaanzishwa Sehemu za Mapitio ( Review Sites) kwenye mtandao, ingawa hizi zilweza kutumiwa kiujanja na wafanyabiashara ambao walifanya kutuma Mapitio yenye kuongea vizuri juu ya biashara zao huku yakiongea vibaya juu ya Washindani wao.

Kutokana na hayo watumiaji wengi wa intaneti wakaanza kugeuka na kutumia Mitandao ya Kijamii ili kupata muda mzuri, habari za ukweli kuhusu taarifa za shughuli na biashara zilizopo katika maeneo yao. Hivyo, Mitandao ikajibu kwa kufanya utumiaji wake kuwa rahisi Kibiashara. Kwa kupatikana na kuunganishwa kirahisi kukaifanya mitandao ya kijamii kuwa eneo zuri kuvutia Wateja wapya katika biashara yoyote. Kadri muda unavyoenda na kukua kwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, kumekuwepo na mahitaji makubwa ya Mameneja Mitandao ya Kijamii (social media managers), ambao wana Utaalamu na Nyenzo za kusaidia wenye mahitaji ya kutangaza shughuli zao kuongezeka.
Kutokana na kuwepo na watu wenye ujuzi wa kutumia Mitandao ya Kijamii, wenye Biashara wameitumia Nafasi hiyo kujitangaza zaidi na kuwafikia Wateja wao kupitia Facebook, Twitter, YouTube, LinkedIn na mingine mingi. Mitandao hii inasaidia kurahisisha mawasiliano na muungano wa manufaa kati ya WafanyaBiashara na wateja wao. ILANI YANGU KWAKO, Mfanyabiashara, Mwenye Viwanda, Taasisi za Kidini, Taasisi za Kibinafsi, Mashirika ya Umma, Mashirika ya Kimataifa, Wanamziki, Wanamichezo na yeyote anayetembelea hapa ni wakati wako wa kujitangaza ili shughuli unayofanya iweze kujulikana na kuongeza kipato kwa kutumia Mitandao ya Kijamii.