Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano ya mtumiaji:Johnjosephtz/yericko nyerere

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Yericko Yohanesy Nyerere (alizaliwa 04 aprili 1983) katika kijiji cha Maduma wilaya ya Mufindi mkoa wa iringa,Tanzania. Alisoma Saikolojia ya kiuchunguzi kutoka katika chuo kikuu huria Uingereza (2016-2017), na akasoma uchunguzi na upelelezi kutoka taasisi ya kimataifa ya Uchunguzi na upelelezi ya International institute of certified forensic investigation professionals inc, kwa kushilikiana na Osulivan Associates International -USA (2015)

Yericko ni mwanzilishi na mfanyakazi wa Kampuni ya YECCO GROUP LIMITED kama mwenyekiti mtendaji. Ni Mwanachama wa Chama cha Kisiasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni muandishi wa vitabu vya vinne Kitabu cha "UJASUSI WA KIDOLA NA UCHUMI," Kitabu cha STRATEGY THE ROAD TO POWER," Kitabu cha MAPAMBANO YA MADARAKA" na Kitabu cha "MTU Baada YA MTU".

Tangu 2010 hadi Julai 2015, Yericko Nyerere alikuwa mshauri wa usalama na Ulinzi binafsi kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt.Wilbrod Peter Slaa. Kama mwanaharakati wa kisiasa anasifika kwa mazungumzo yake ya busura juu ya mabadiliko ya kisiasa na maendeleo ya kiuchumi nchini Tanzania, kazi zake hasa vitabu na makala mitandaoni zimesababisha ushawishi mkubwa kwa kura nyingi kwa watoa maamuzi na viongozi wa kisiasa. Amekuwa msukumo wa kisiasa kwa mabadiliko na ushiriki wa vijana na ushiriki katika ajenda ya serikali na mabadiliko ya kiuchumi.

Urithi wake wa fasihi juu ya uandishi pia unadhihirishwa juu ya mkakati wa ushindi wa ushirika wa vyama wa vyama pinzani nchini Tanzania (UKAWA) wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015, ambapo aliiandika mkakati huo ambao baadae aliufanya kitabu cha Strategy.


vyanzo https://searchworks.stanford.edu/view/12863187

https://www.distansce-learning-centre.co.uk/products/306/forensic-psychology-diploma-course.htm

http:www.open.ac.uk

http:www.crd.go.tz/yeccot-limited [1] [2] [3]

http:www.chahali.com/2013/08/uchambuzi-wa-mwanaharakati-yericko.html?m=1

http:www.mwananchi.co.tz/habari/kitaifa/Yeriko-Nyerere-afikishwa-mahakamani-/1597296-2940666-e14dxy/index.html [4] [5]