Majadiliano ya mtumiaji:FRATE MUSHI

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
                    ===== SHABU =====

Shabu ni aina ya madini ambayo yanachimbwa ardhini, yana rangi nyeupe kama chumvi au chokaa, shabu ilianza kugundulika huko ufilipino kama tiba mbadala pia wengi walikua wakitumia kama madawa ya kulevya yakiwa na kiasi kidogo sana pia ikawa inatumika kama dawa ya kusafishia maji machafu ambapo ukiiwekwa ndani ya maji machafu kwa rangi au yenye matope baada ya muda mfupi yanabadilika na kuwa meupe au masafi, utaalamu huo ukafika mpaka Afrika, Kwa Tanzania Shabu inatumika sana kanda ya ziwa (yaani Mwanza, Shinyanga, Geita kwa sasa na maeneo yote yanayo lizunguka ziwa Victoria pamoja na Kigoma) na maeneo ya Pwani yaani kando kando ya bahari.

matumizi ya Shabu yakazidi kuongezeka ambapo kwa sasa inaweza ikatumika kama dawa ya kutibu vipele vya ndevu ili limekua tatizo kubwa hasa kwa wanaume wengi kupata vipele wakati wa kunyoa, vipele hivyo huwatokea pindi wamalizapo kunyoa na kwa wengine huwa vikubwa kama majipu na pia hukifanya kidevu kuwa cheusi mpaka kwenye mashavu, pia hufanya eneo lililoadhirika kuwa ligumu sana, kwa matatizo yote hayo shabu inayouwezo wa kuondoa vipele sugu vilivyopo eneo la kidevu au vinavyotokea baada ya kunyoa hivyo shabu inayo uwezo wa kutumika pia kama After shave, pale muhusika anapomaliza kunyoa anawza kupaka Shabu badala ya After Shave na ikamsaidia kuondoa kabisa uwezokano wa vipele kuota na kuondoa ambavyo vilikua vimeshaota kidevuni na maeneo ya mashavu. pia ina uwezo wa kuondoa fangasi katika sehemu zote za mwili kama miguu, mikono, kichwani, sehemu za siri pamoja na maeneo yote ya mwili wa binadamuna kuurudisha mwili katika hali nzuri zaidi