Majadiliano ya mtumiaji:Dismas Lyassa

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Dismas Lyassa ni mwandishi wa habari maarufu Tanzania, aliyezaliwa Juni 26, 1976 katika kijiji cha Mofu, mkoani Morogoro, wilayani Kilombero.

Amesomea mambo mbalimbali yakiwemo storekeeping kutoka chuo cha Biashara (CBE), pia kule Kenya ambako alipata elimu ya uandishi wa habari (Advanced Diploma in Journalism and Mass Communication).

Akiwa Kenya katika Jiji la Nairobi makazi yake yalikuwa Ngara men's Hosteli, ambako baadaye aliandika kitabu juu ya vyakula vizuri na vibovu alivyokuwa akila Kenya.

Alisema pia kwamba kupitia kusoma Kenya amejifunza kwamba kuna baadhi ya vyakula ni muhimu sana katika maisha ya mwanadamu kuliko vingine. katika kitabu chake cha saikolojia na utafiti sehemu ya pili, Dismas Lyassa, baba mwenye watoto wawili (Gloria aliyezaliwa 7/7/2001 na Godfrey 30/10/2002) anasema baadhi ya vyakula alivyokuwa akivila pale Ngara hakuvipenda, lakini alishangaa kuona ananawili.

"Kuna vyakula kadhaa vilikuwa vinanipa kuvira...lakini nashangaa nikawa mwenye afya nzuri, hata nilivyorudi Dar es Salaam, afya yangu ilikuwa nzuri na kwa ujumla nilipendeza," anasema.

Umaarufu wa Dismas Lyassa ambaye amemuoa mchungaji Rightness toka Machi 30 2001 pale Kanisa la Roman Cathoric wakati huo akiabudu kanisa la Roma, unatokana na uwezo wake mkubwa katika kushauri kwa njia ya maandishi; ana safu nyingi za ushauri wa masuala ya vijana na ndoa.

Ana safu ya ushauri wa ndoa katika gazeti maarufu na linaloongoza kwa mauzo Tanzania, Mwananchi, kila Jumapili, pia gazeti linaloongoza kwa mauzo kwa upande wa magazeti ya wiki Mwanaspoti, kila Jumanne. Pia ana safu katika gazeti la Mwananchi alhamisi kuhusu masuala ya uchumi na biashara. Zaidi ya hayo amewahi kuandika vitabu vingi kuhusu saikolojia na utafiti, ameandika pia kuhusu ndoa nk.

Mkewe Rightness kwa sasa ni mchungaji, kazi ambayo anasema alishauriwa na Dismas mwenyewe. Wakati wanaoana Dismas alikuwa Roma na mkewe alikuwa muumini wa KKT, lakini baadaye kwa pamoja wakabadilisha dhehebu na kuamua kuokoka. Mkewe kwa ujumla amekuwa ni mtu mwenye kupenda kumtumikia Mungu zaidi, huku Dismas akijishughulisha zaidi ya kazi za uandishi wa habari.

Dismas amewahi kuwa mshindi wa tuzo ya uandishi wa habari bora Tanzania )print-media 2007 katika tuzo ya Edward Moringe Sokoine. Pia amewahi kuwa mhariri/mtafiti wa mashirika mbalimbali ya ndani ya nje.

Anafahamika kwa uwezo wake mkubwa wa kuandika mambo yenye kugusa jamii, ndio maana hata unapotafuta mambo mbalimbali kwenye internet kuhusu maisha na ndoa, ni nadra kukosa makala za Dismas Lyassa.

Ameruhusu watu kuzitumia watakavyo, ili mradi wasibadilishe maana au kuharibu maudhui yake. Tangu mwaka 2001 licha ya kuajiriwa katika magazeti mbalimbali kwa nyakati tofauti kama mhariri wa makala gazeti la Leo ni Leo, mhariri mtendaji wa magazeti ya udaku ya Fukuto, Risasi nk, licha ya kuajiriwa kama mhariri mkuu wa gazeti la Uwazi kutoka 2003 hadi 2005 alipohamia gazeti la mwananchi kama mwandishi wa makala, pia amekuwa akimiliki shughuli zake binafsi.

Ana ofisi yake barabara ya Mandela, karibu na hoteli ya Landmark, Ubungo. Pamoja na mambo mengine amekuwa akikutana na watu mbalimbali kwa ajili ya kuwapa ushauri wa maisha, ndoa na biashara.

Aidha amekuwa mwakilishi wa vyuo mbalimbali vya nje ya Tanzania, baadhi yake ni Ireland International kilichoko Ireland, European University kilichoko Uswis, Singapore, Spain, UK, Austria nk.

Agombea Ubunge

Mwaka 2015, Dismas Lyassa aligombea Ubunge katika kura za maoni ndani ya jimbo la Mlimba lililotokana na kugawanywa jimbo la Kilombero, mkoani Morogoro. Alifanikiwa kufanya vizuri kwa nafasi ya nne, huku mwenyewe akinuliwa akisema amepata kura NO; Akimaanisha Next Opportunity.

Akiwa katika mkutano wa kumnadi mgombea Ubunge katika Jimbo la Kilombero, Abubakar Assenga, mwanasiasa huyo ambaye kimuonekano si mzungumzaji sana, alisema maneno machache kwamba anafurahi kupata kura za NO na kwamba anaamini waliompa kura hizo walikuwa na akili timamu, hivyo anawaomba wananchi hasa wanachama wenzake wa CCM kushirikiana kumnadi mgombea ambaye sasa ndio anagombea katika nafasi ya Ubunge katika Jimbo hilo.

Dismas Lyassa amewahi kumiliki gazeti alilolipa jina la Jiamini (Confident) lililotoka mara kadhaa kabla ya mwenyewe kulizuia akisema kwamba kuna mambo anataka kujipanga zaidi kabla ya kuja upya. Hata hivyo wengi wamekuwa na shauku kubwa kuona anakuja vitabu, huku mwenyewe akisema anataka kuja na vitabu, gazeti na redio.