Majadiliano ya msaada:Contents

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

[[ na allen kilewella}]]

kupatikana kwa blogu na jitihada za ndesajo macha kutuelimisha juu ya matumizi ya zana hii muhimu kwa kuombozi wa watu maskini duniani,ni jambo linalotakiwa kuchukuliwa kwa uzito wa hali ya juu!

lakini kwa nchi kama ya kwetu tanzania ambayo kwa kiasi kikubwa watu wake bado hawajaweza au hawana hamu ya kujiingiza katika matumizi ya teknolojia hii kunahitajika juhudi za ziada kuhamasisha hasa vijana kutumia migahawa ya internet kwa manufaa zaidi kuliko ilivyo sasa.

unaweza kuangalia vijana ukagundua kuwa wengi wao wamekata tamaa ya kutafuta maarifa kwani hawajui hata wakiyapata watayatumia wapi! muda mwingi wanaotumia katika migahawa ya Internet wanautumia kwa kuangalia ponografi na kusikiliza muziki wa Bongo Fleva au muziki wa rap kutoka marekani.

jitihati kama za kina Ndesajo kutumia magazeti kutoa habari za blogu zinatakiwa kuungwa mkono na magazeti mengine mbali ya gazeti la mwananchi ambalo macha analitumia.

hali ya mambo hapa nyumbani tanzania si shwari. uzalendo umekufa kwa asilimia tisini (90%) na asilimi kumi iliybaki iko kwa jamii isiyo na uwezo wa kumiliki vyombo vya habari. vyombo vya ahabari tanzania vinatumika kama vitanzi vya kunyonga akili na fikara za wapiga kura wakati wa uchaguzi.

Baada ya uchaguzi kupita vyombo vya habari hugeuka na kuwa mabaraza ya kupiga porojo na kujenga taswira hasi kuwa wananchi wanatekelezewa kila kitu walichoahidiwa na wanasiasa wao! ni kawaida kwa asilimia mpaka ya themanini (80%)ya habari zinazotoka kwenye vyombo vya habari baada ya uchaguzi zinatokana na warsha,semina,hotuba za wanasiasa,habari za kipolisi huku habari kosoaji zikisemwa na waharirikuwa haziuzi " habari ". hapo ndipo umuhimu wa blogu unapoonekana