Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano ya kigezo:Muigizaji

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwanza kuna kitu kinanishangaza, Kwanini haitaki kuonyesha ile sehemu ya jina la kuzaliwa?--Muddyb Blast Producer 11:46, 22 Oktoba 2007 (UTC)[jibu]

Tatizo kubwa lipo kwenye jina la kuzaliwa haitaki sijafahamu kwanini kwanini haitaki.--Muddyb Blast Producer 12:19, 22 Oktoba 2007 (UTC)[jibu]

Sijaelewa bado tatizo. Mimi naona mstari:
| jina la kuzaliwa =
Kwani usiingize katika makala halafu tuone? --Kipala 12:21, 22 Oktoba 2007 (UTC)[jibu]


Nimejaribu bosi hilo naomba nisadie, Kama kuingiza katika makala nisha jaribu lakini sikufaulu.--Muddyb Blast Producer 12:27, 22 Oktoba 2007 (UTC)[jibu]

Naomba uangalie Bud Spencer. Tatizo la
| jina la kuzaliwa =
ilikuwa jambo dogo ulikuwa umeandika "jinalakuzaliwa" katika mabano ya mkia yaani {{ hivyo bila kuacha nafasi "jina la kuzaliwa". Ila tu sieelewi kwanini inameza sasa orodha ya yaliyomo nadni yake? Sijui una amri ya TOC katika templeti? Menginvyo jaribu kwanza kuweka vipengele vongine halafu hifadhi na tuone. --Kipala 12:35, 22 Oktoba 2007 (UTC)[jibu]

Bado sijafahamu nini maana TOC?--Muddyb Blast Producer 12:42, 22 Oktoba 2007 (UTC)[jibu]

TOC ni kifupi cha Table of Contents lakini hii haikuwa tatizo. Nimesahihisha mwisho wa templeti ilitakiwa kuwa |} badala ya }}. --Kipala 12:49, 22 Oktoba 2007 (UTC)[jibu]

Kuna mauzauza (Miracles) mengine mwisho wa template kuna ala ya # kisha lile neno tovuti lajitokeza lenyewe bila kupewa amri ya kutokeza je hilo nalo vipi?--Muddyb Blast Producer 13:07, 22 Oktoba 2007 (UTC)[jibu]


Muddy, nimeangalia kidogo templeti hii. Unajua mimi si mtaalamu sana katika habari za templeti nimekanyaga hatua chache tu. Lakini ninavyoona umechukua sampuli ngumu kidogo ambayo ni ya kutatanisha kidogo. Ukitaka ushauri wangu heri uende na mfano rahisi zaidi. Ni swali la muundo.

Nimelinganisha na template:elementi niliponakili muundo nyepesi zaidi. Kama muundo ni nyepesi hatari ya makosa yapungua. Kwa bahati mbayo umefuata mfano mwenye tego ndani yake.

Muundo nyepesi ni: a) kila kipengele kuwa na mistari mitatu tu inayotenganishwa na alama "|-":

|-
{{#if: {{{jina}}}|  
{{!}} '''Jina'''    
{{!}} {{{jina}}}}}  
|-

b) Kujitahadhari kuhusu mabanao ya mkia }} kwa sababu haya ni amri kwa programu.

  • Kutoingiza mabano ya mkia ndani ya mabano ya mkia kwa sababu sina uhakika hii inafanya nini.
  • Pia kutumia mabano haya kama {{{jina}}} mara moja tu kila mstari. Sijui kabisa safari ya pili inafanya nini.
  • kwa hiyo kutorudia mabano ambayo huelewi au pia amri nyingine za katikati kama vile |<span class="label">.

c) Kimsingi ushauri wangu ni

  • chukua templeti inayofanya kazi kama "elementi" - wacha mifano mingine ambayo ni kubwa na ya kutatanisha kutoka en:wiki
  • panga habari unazotaka kutaja ni ng'api.
  • ongeza au kupunguza idadi ya vipengele kama a) kulingana na iadda inayotakiwa
  • halafu andika maneno yako ndani ya mabano yaliyopo badala ya maneno ya "template:elementi"
  • kakikisha yafuatayo katika kipengele:
    • mabano ya mkia ya mstari wa kwanza (inayoanza kwa #if:) na wa tatu yalingane kabisa !
    • kwenye mstari wa pili andika yale unayotaka kuona kwenye ukurasa
    • halafu tengeneza jedwali la juu kati ya amri za <pre> / </pre> na hapo chukua maneo kwa tahajia kamili ya yaliyomo ya mstari wa tatu.

Ni haya tu. Pole sana! Utashinda, Bwana, najua - --Kipala 13:32, 22 Oktoba 2007 (UTC)[jibu]

Hivyo ni vita vya kizamani hasa wamarekani walikuwa wakipigana vita huku wakirudinyuma (Retreat). Mfano wako ni mzuri lakini tayari nimesha anza je itakuwaje? Maana kuanzisha template upya sio mchezo mzee wangu, Inauma sana yaani. Kama vipi tujaribu kwa mara ya mwisho, Naomba nifutie yale maandishi: mahali pa kaburi, influence na mengine ambayo hayana ulazima tafadhali.--Muddyb Blast Producer 14:04, 22 Oktoba 2007 (UTC)[jibu]

Muddy wasema hii templeti yakupa matatizo. Siwezi kuitambua nikifungua ukurasa unaotumia templeti kama Stephen Kanumba. Tujaribu screenshot. Mimi hufanya screenshot kwa kufungua ukurasa ule unaotaka kuinionyesha.
Kama hujafanya kazi hii bado hapa maelezo:
  • Bofya "print" (kwa kawaida juu upande wa kulia kwenye sehemu ya kinanda),
  • halafu fungua programu kama "paint" (ama kupitia Start-All Programmes-Acessoires-paint AU kupitia tart-(execute /sijui neno lake ni dirisha ndogo la kuweka amri)- mspaint).
  • Katika paint unaingiza picha ya dirisha la awali kupitia "paste".
  • Sasa unakata sehemu ile tu ambayo unaitaka kunionyesha halafu unainakili na kuiweka kwa ukurasa mpya.
  • Ukurasa huu unahifadhi kama picha.
  • Baadaye pakia katika sw:wiki na kuingiza hapa. Ukihariri picha unaweza pia kuchora duara nyeupe mahali unapoona si sawa. --172.174.15.67 09:40, 24 Oktoba 2007 (UTC)[jibu]

Hiyo ni habari nzito. Kwanza hiyo screeshot sijaelewa vizuri namna ya kufanya, Kila nikifanya naona haitaki je nifanye? Tafdhali nitajie njia nyingine. Kuhusu maelezo bwana kipala huwezi kuelewa mpaka ulinganishe kurasa yaani inabidi ufungu kurasa ya makala yenye template ya msanii muziki, Kisha ufungue makala yenye template muigizaji, hapo tofauti utaiona. Hebu jaribu fungua hii kisha fungua na hii kwa wakati mmoja ufungue dirisha mbili kisha fananisha utaona kuna moja habari na template zimeshuka chini kidoogo badala ya kichwa cha habari ya makala, Hiyo ni ile ya muigizaji tafdhali fungua utaona kasoro kuna moja haijaanza sahihi. Tuendelee--Muddyb 12:43, 24 Oktoba 2007 (UTC)[jibu]

Screenshot: kama unatumia mashine kwenye internet-cafe labda walisimamisha nafasi hii. Je unaweza kubonyeza print na inasema nini? (ukijibu kwa screenshot yako futa picha yangu tusijaze ukurasa mno)
Halafu: bado sijaelewa tatizo ni nini. Sawa kuna tofauti ndogo lakini je kuna ugumu gani? Tofauti labda imepotea sasa (kama nimekuelewa vema!) kwa sababu niliingiza templeti moja maelezo na jedwali kama katika templeti nyingine.--Kipala 13:27, 24 Oktoba 2007 (UTC)[jibu]

TABASAMU KUUBWA, Nd. kipala sina la kusema. kwa kweli umenimaliza sana juu ya hili tukio la Screenshot, Sijawahi kuona hii ni kwa mara ya kwanza ni kwako kuona na kusikia pia. Kuhusu mashine: kwani unazani ninahela gani za kukaa internet cafe kuanzia asubuhi mpaka jioni, Mimi natumia mashine ya kampuni ndiomaana nina mda hata wa kuahariri makala kutokana internet silipii ni tajiri yangu ndiyo anaelipia. Kama kuna uwezekano wa kuwa na chochote kile kilitokea katika mashine mie sijui labda muajiliwa wa kwanza aliyekuwa anatumia mashine hii ndio kafanya hivyo ila mie kwangu safi tu isipokuwa nikibonyeza Print hamna kinachotokea zaidi ya kuwa kimya, je ipo namna ya kufanya ili iweze kufanya screenshot? Naomba nitajie alama zenyewe za kuwekea screenshot, Mimi nahisi zimeandikwa: Print Screen, Sys Rq ndio hivyo? --Muddyb 14:06, 24 Oktoba 2007 (UTC)[jibu]

Muddy pole sana hongera na mwajiri anayevumilia shughuli za wikipedia. Sasa kuhusu screenshot: ni kweli ya kwamba hakuna kitu kinachoonekana ukibonyeza "print". Ila tu umechukua picha ya dirisha iko ndani ya kumbukumbu ya mashine (sawa kama kunakili kwa kutumia panya yako kwa copy/paste maana inabaki tu hadi utakapozima au kunakili kitu kingine). .
Baada ya kubofya "print" una fungua programu (kwa mfano paint - usipoikuta fanya jaribio kwa Word hata kama haisaidii kwa wikipedia) na hapa unapakiza (kwa menu edit-paste AU kwa panya rightclick-paste AU kwa kushika CTRL halafu bofya V). Jaribu tu. Ila tu usihifadhi hii ni format ya bmp na faili kubwa sana; katika paint au programu nyingine ya picha unaweza kuchagua ".jpg" . --172.181.245.154 14:32, 24 Oktoba 2007 (UTC)[jibu]

Screenshot / picha ya kiwamba

[hariri chanzo]

Screenshot ni picha la kiwamba au skrini ya kompyuta. Ni rahisi kabisa hata kama haijulikani kwa watu wengi sana. Inasaidia maelewano kati ya watumiaji wa mtandao kwa sababu picha hii inawezekana kuhifadhiwa na kutumwa kwa email au kuitumia kwa wikipedia.

Namna ya kufanya picha ya kiwamba

[hariri chanzo]
  1. Chagua ukurasa au mwandishi au yale unayotaka kuonyesha na hakikisha yameonekana kwenye kiwamba cha komyuta yako
  2. halafu fungua programu ya picha - kwa mfano "paint" (ama kupitia Start-All Programmes-Acessoires-paint AU kupitia tart-(execute /sijui neno lake ni dirisha ndogo la kuweka amri)- mspaint).
  3. Kwenye dirisha unalotaka kuonyesha bofya "print" (kwa kawaida juu upande wa kulia kwenye sehemu ya kinanda). Hutaona badiliko lakini umenakili tayari picha ya skrini yako katika kumbukumbu ya muda.
  4. Katika paint (au programu nyingine ya picha) tekeleza amri ya "paste" (kwa menu edit-paste AU kwa panya rightclick-paste AU kwa kushika CTRL halafu bofya V).
  5. Amri hii inaingiza picha ya kiwamba katika dirisha la paint.
  6. Picha hii awali bado si imara, unaweza kuisukuma. Bofya "Esc" halafu ni imara.
  7. Sasa unakata sehemu ile tu ambayo unaitaka kuonyesha halafu unainakili na kuiweka kwa ukurasa mpya ya paint.
  8. Ukurasa huu unahifadhi kama picha ukichagua fromat ya jpg.
  9. Ukihariri picha unaweza pia kuchora duara nyekundu mahali unapotaka kuonyesha hasa.
  10. Hii faili ya picha unaweza kutuma kwa barua pepe au kuingiza katika wikipedia.

TAHADHARI: Usisahau kubadilisha format kuwa jpg au kile unachotaka kwa sababu pekee yake ni faili kubwa sana ya format ya bmp.

Majibu ya picha ya Kiwamba

[hariri chanzo]

Mwajiri wangu hastairi hongera hata kidogo isipokuwa mimi mwenyewe naweka taratibu zangu vizuri najibana huku na huku ili niweze kufanya kazi na Wikipedia na pia kwa mwajiri wangu hivyo pongezi zote nazibeba mwenyewe tajiri haambulii hata moja, Katika pongezi ulizotoa. Kuhusu sreenshot hebu angalia tofauti iliyoko kati ya sw-wiki na en-wiki:

Mimi naona sawa

Hebu angalia vizuri, Kama aina ulazima wowote sawa lakini habari ndio kama unavyoiona. Kumbuka kuhusu Wikipedia ni mimi mwenyewe ninayefanya kazi hizi kisha nafanya kazi muajiri wangu. Kazi ninyofanya kwa muajiri wangu ni shughuli kihasibu niko namsaidia muhasibu kufanya kazi fulani hivi ambazo mimi zimeniweka pale. Kwa kunifanya nisiumie kichwa sana wameniwekea internet kisha wao wakaitoa yaani walipunguza Bandwidth. shida yao hasa mie niwe natumia mtandao wa skype basi na sio mitandao mingine. Baadae nikaja na Program iitwayo Mac address changer hiyo ndiyo niliotumia kuongezea Bandwidth, Ndiomaana mpaka leo hii niko na nyinyi wikipedia lakini bosi hajui kama mimi nina internet kama unavyojua wahindi hawataki watu weusi tuwe na internet wakaamua kunipungua Bandwidth. kwa uwezo wangu wa fikra na ufahamu wa Program za Mahakers nikatumia Mac Address Changer hivyo nimempiga bao muhindi ujanja hana tena mimi najifanya mjinga kumbe mjanja sivyo kama alivyokuwa anafikiria mpaka leo hii nina internet na nitandelea kuweka makala na kuindeleza Wikipedia mpaka siku nitakayondoka hapa. Sujui lini na mwaka gani lakini Wikipedia siiachi milele. Tuombeane kheri ili Wikipedia tuipeleke mbali unasemaje? --Muddyb 15:18, 24 Oktoba 2007 (UTC)[jibu]

Muddy, nakutakia kila ya kheri. Sasa nimebadilisha sreenshot na kuweka picha kando. Sioni tofauti isipokuwa en:wiki wana nafasi kubwa zaidi juu kwa matangazo na kadhalika. Ukitumia mstari juu ya mwandishi kama msingi ni hivihivi. Basi lakini naondoka sasa. --Kipala 15:29, 24 Oktoba 2007 (UTC)[jibu]