Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Vivumishi vya pekee

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Vivumishi vya pekee vimekuwa vikileta hali ya kutokuwa bayana kwa wanasarufi wengi. Vitabu vingi vielezavyo dhana ya vivumishi hasa katika daraja la vivumishi vya pekee, waandishi wake yamkini hawajafanya uchunguzi wa kutosha. Neno pekee katika aina hii ya vivumishi linatokana na Aina ya nomino za pekee hasa zile ambazo ni majina ya pekee ya mahali kama vile Afrika, TAnzania, Kilimanjaro, Dar es Salaam, New York, London n.k. Kivumishi cha pekee kinachotakana na Nomino ya pekee ya Afrika ni Muafrika kama tunazungumzia mtu au kiafrika kama tunazungumzia kitu kischo mtu. Tanzania inatupatia kivumishi cha pekee Mtanzania / Kitanzania. Wingereza inatupatia kivumishi cha pekee cha Mwingereza / Kiingereza n.k. Hii ndiyo hasa halisi ya aina ya vivumishi viitwavyo vya pekee.

Mifano katika sentensi: Tafadhali nipimie mchele wa kijapani kilo saba. Utamaduni wa kiafrika ni tofauti kabisa na utamaduni wa Kiulaya. Nyimbo za kinaijeria huimbwa katika lugha ya wazawa. Maneno: kijapani (Japan), Kiafrika (Afrika) na kiulaya (Europe)yametumika kama vivumishi vya pekee. Hii ndiyo maana nimetangulia kwa kusema neno "pekee" katika "vivumishi vya pekee" limetumika kuonesha kuwa vivumishi hivi vimechimbuka kuto "Aina za nomino za pekee za mahali"

Start a discussion about Vivumishi vya pekee

Start a discussion