Majadiliano:Vielezi
Mandhari
Vielezi ni maneno yanayoelezea tendo lilivyofanyika au litakavyofanyika.Vielezi hufafanua kitendo kilitendeka wapi,vipi,mara ngapi na namna gani.
Aina za vielezi
[hariri chanzo]Kuna aina nne 4 za vielezi.aina hizo ni:
- (i)Vielezi vya namna au jinsi
- (ii)Vielezi vya mahali
- (iii)Vielezi vya idadi
- (iv)Vielezi vya wakati
(i)Vielezi vya namna au jinsi
[hariri chanzo]Ni aina ya vielezi ambavyo huelezea namna au jinsi ya kutendeka kwa tendo. Vielezi hivi huelezea jinsi gani tendo hilo limetendeka.
(ii)Vielezi vya mahali
[hariri chanzo]Ni aina ya vielezi ambavyo huelezea mahali kulikotendeka tendo.Vielezi hivi hueleza tendo hilo limetendeka wapi.
(iii)Vielezi vya idadi
[hariri chanzo]Ni aina ya vielezi ambavyo huelezea idadi ya kutendeka kwa tendo.Vielezi hivi hueleza tendo hilo limetendeka mara ngapi.
(iv)Vielezi vya wakati
[hariri chanzo]ni aina ya vielezi ambavyo hueleza wakati wa kutendeka kwa tendo.Vielezi hivi hueleza ni lini hasa tendo hili limetendeka.