Majadiliano:Ukristo nchini Kenya

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ukristo nchini Kenya kwa jumla unaishi kwa amani, ukitumia uhuru wa dini unaohakikishwa na katiba ya mwaka 2010.

Hata hivyo miaka ya hivi karibuni baadhi ya Wakristo waliuawa na wafuasi wa Al Shabaab.

Upande wa takwimu, kulingana na sensa ya mwaka 2009, Wakristo walikuwa asilimia 82.5 ya wakazi wote wa Kenya (asilimia 47.4 Waprotestanti, asilimia 23.3 Wakatoliki, asilimia 11.8 Wakristo wa madhehebu mengine mbalimbali). Utafiti mwingine pia umeonyesha kuwa Ukristo ndio dini kuu ya wakazi wa Kenya (84.8%)[2][3].

Wakristo 70,000 hivi walitokea familia za Kiislamu.[4] [[Jamii:]]dini