Majadiliano:Papa Valentino
Mandhari
Tarehe ya kufariki kwake
[hariri chanzo]Ingawa wikipedia ya Kiingereza inataja tarehe ya kufariki kwake Papa Valentino kuwa 16 Septemba 827, haileti maana kwa vile inasema kwamba alikuwa papa kwa siku 30 au 40 kuanzia tarehe 1 Septemba (tarehe ya uchaguzi wake haiwezekani kuwa mapema zaidi kwa vile Papa Eugenio II, mtangulizi wake Valentino, alifariki tarehe 27 Agosti tu). Kwa hiyo nimefuata Kamusi Elezo ya Kikatoliki inayosema kwamba Papa Valentino alifariki mwezi wa Oktoba, na tarehe kamili haijulikani. Yeyote ambaye angeweza kutaja tarehe ya kufariki kwa Papa Valentino na uhakika mkubwa zaidi aitaje hapahapa (pamoja na kiungo au rejeo linalothibitisha tarehe hiyo). --Oliver Stegen 13:23, 19 Julai 2007 (UTC)