Majadiliano:Ntobo (Igunga)
Haya ni Majadiliano kwa ajili ya kuboresha makala ya Ntobo (Igunga). | |||
---|---|---|---|
|
|
Hii ni makala ya Ntobo (Igunga) ipo katika eneo la Wikipedia:Mradi wa Tanzania, juhudi za pamoja katika kuboresha maeneo ya Tanzania kwenye Wikipedia. Iwapo utapenda kushiriki, tafadhali tembelea ukurasa wa mradi, ambapo unaweza kujiunga na majadiliano na utazame orodha ya kazi zilizo wazi. |
Igunga
[hariri chanzo]Igunga ni kijiji kilichopo magharibi mwa wilaya ya Igunga mkoani Tabora Kaskazini mwa barabara kuu itokayo Igunga kwenda Nzega. Kijiji hiki kinapakana na vijiji vya Mwamilu kwa upande wa kusini; kijiji cha Ngulu upande wa kusini magharibi; kijiji cha Imalilo kwa upande wa magharibi na kijiji cha Mwamloli kwa upande wa Kaskazini. Upande wa Mashariki kijiji cha Ntobo kinapakana na kijiji cha Mwabubele.
Kijiji cha Ntobo vilevile kinabeba jina la kata ya Ntobo. Kata hii inaundwa na vijiji vinne ambavyo ni Ntobo, Mwamloli, Mwabubele na Mwamilu. Kiutawala, ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata (WEO) ya Ntobo ipo katika kijiji cha Mwamilu. Vilevile ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kijiji (VEO) nayo ipo katika kijiji cha Mwamilu. Kwa muundo uliopo, kijiji cha Mwamilu hakina ofisi ya serikali ya kijiji wala kata japokuwa ofisi zote mbili, ya WEO na VEO Ntobo, zote zipo katika kijiji hiki cha Mwamilu lakini hakuna ofisi inayobeba jina la Mwamilu.
Kata ya Ntobo imo katika tarafa ya Igurubi na ni miongoni mwa kata 26 zinazounda Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Shughuli kuu za uchumi katika kata ya Ntobo ni kilimo na ufugaji. Mazao makuu ya chakula ni mahindi, mtama, karanga, viazi vitamu, mpunga, njugu mawe, choroko na kunde. Wakazi wa kata hii hujihusisha na ufugaji wa ng'ombe, mbuzi, kondoo, kuku na punda.