Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Muhammadu Buhari

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Muhammadu Buhari (amezaliwa tar. 17 Desemba 1942) amekuwa rais wa Nigeria tangu 29 Mei 2015. Anashika cheo mara ya pili maana aliwahi kuwa rais toka 31 Desemba mwaka 1983 hadi 27 Agosti mwaka 1985. Wakati ule aliingia madarakani kama jenerali ya jeshi kwa kumpindua rais aliyechaguliwa Shehu Shagari. Buhari mwenyewe alipinduliwa mwaka 1985 na jenerali Ibrahim Babangida.

Katika kura za uchaguzi za miaka 2003, 2007 na 2011 aligombea urais bila kufaulu. alikuwa mgombea urais katika uchaguzi wa kitaifa wa mwaka huo, lakini hakuibuka kuwa mshindi. Alirudia kugombea katika kura ya mwaka 2015 aliposhinda dhidi ya rais Goodluck Jonathan kwa asilimia 54 za kura zote.[1]

Muhammadu Buhari katika awamu la kwanza la urais alitanguliwa na Shehu Shagari kisha akafuatiwa na Ibrahim Babangida.

Start a discussion about Muhammadu Buhari

Start a discussion