Majadiliano:Moshi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Salamu kwa mpenda Moshi[hariri chanzo]

Naona mwenzetu asiye na jina ameanza kuchangia kuhusu Moshi. Karibu sana! Ila tu tukumbuke ya kwamba hii ni kamusi si gazeti. Hivyo lugha ilingane. "Tunapata fedha za kigeni kwa maendeleo ya mji wetu. wamanchi wanafanya kazi sana wamama wazazi wanakula kitawa na mtori. moshi ni mji wenye baridi sana"

Haya yote ni hoja nzuri ila tu lugha hailingani na masharti ya kamusi elezo. "Tunapata fedha" - haieleweki ni nani kwa sababu hatuandiki majina yetu humo. Mimi sipati fedha. "moshi ni mji wenye baridi sana" ni sawa kwa mtu wa Unguja anayetembelea mwezi wa saba - lakini si kweli hata kidogo katika kamusi mtandaoni inayosomwa na mtu wa Chicago au wa Norwei penye baridi kweli.

Naomba ujaribu kuisahihisha mwenyewe - au sisi wengine tutasaidia karibuni. --Kipala 14:16, 14 Septemba 2006 (UTC)[reply]