Majadiliano:Mkotokuyana

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Palikuwa na fundi mhunzi wa kabila la Wamwera. Fundi huyo jina lake aliitwa MKOTO maana yake kwa lugha ya kimwera ni MZURI au VIZURI. Fundi huyo alikuwa hodari sana na maarufu sana kutokana na kufanya kazi zake vizuri hususani ufuaji wa Majembe na Mashoka. Katika barabara yakwenda kwa fundi MKOTO kulikuwako na mzee mmoja ambae pia ni wa kabila la Wamwera. Mzee huyo alikuwa na tabia ya kumuuliza kila mtu anayepita njia hiyo kuwa anaenda wapi lakini kwa kutumia lugha ya Kimwera. Swali lake mara zote lilikuwa hivi: "Kuukwenda kwei?" yaani Unakwenda wapi?. Sasa kwakuwa ile ilikuwa ni njia pekee yakwenda kwa mzee MKOTO, na kwakuwa watu wengi walikuwa wanakwenda kwa MKOTO kwa sababu ya kufua majembe, na kufua kwa Lugha ya Kimwera ni 'KUYANA' hivyo basi maranyingi majibu yalikuwa yanafanana. Majibu yenyewe ni "Kuungwenda kwa MKOTO-KUYANA Majela gangu" maana yake ni: naenda kwa fundi MKOTO Kufua majembe yangu. Au wakati mwingine walijibu hivi "Kuungwenda kwa MKOTO KUYANA mabago gangu" maana yake naenda kwa MKOTO KUFUA Mashoka yangu n.k. Kwa kuwa ilizoeleweka jina MKOTO na lile tendo la kufua (KUYANA) zana za kilimo, mnamo mwaka 1975 waliamua kwa pamoja jina la kijiji hicho liwe "MKOTOKUYANA" ikiwa na maana "KUFUA VIZURI" kwa heshima ya huyo fundi Majembe Mzee MKOTO. Historia hii ilitolewa na kusomwa na Hayati Mzee JUMA NAMANGUKU maarufu kama Mpishi Juma. Mimi ni: THOMAS GEORGE MMUNI; Ni mzaliwa wa Mkotokuyana, Nimekulia na kusoma hapo. Simu +255765-941752 au +255714-259674 Email.(1) mmuni1981@gmail.com

    (2) thomasnchumari@yahoo.com