Majadiliano:Mbuzi-kaya
Ndugu uliouanzisha makala hii ya Mbuzi, unaombwa uwe na busara katika masuala yako unayoyafanya. Tunafurahia kuona mtu mpya anaingia na kuchangia makala katika Wikipedia hii ya Kiswahili, ila tu uhuni hautakiwi.
Iweje uunde makala kisha aje mwingine kusawazisha kisha wewe ufute yale maelezo na urudishe kama awali? Kitendo hicho sio kizuri kabisaa, na inabidi ubadilike na ukumbuke kwamba hii ni kamusi elezo huru kila mtu anaweza kuhariri.
Endapo mimi nitakosea ukija wewe utasawazisha na mimi nikikuta masaawazisho hayo wala sinto thubutu kufuta. Hivyo waombwa uwe na uvumilivu na wala usijikie vibaya pale ukiona makala uliochangia akatokea mwingine na kuibadilisha au hata kurekebisha katika mwelekeo mzuri.
Haya, nilikuzuiya kuhariri Wikipedia kwa muda wa siku moja, lakini naona haina haja tufanyiane hivyo ilhali wote sisi ni wachangiaji. Hivyo nakufungulia na uendelee kuchangia katika Wikipedia hii ya Kiswahili. Ushauri: Ni vyema kujiandikisha kulikoni kuchangia bila jina. Moja, IP address yako inaonekana dhahiri, na mbili kurahisisha mawasiliano baina mtu na mtu.
Naomba ujiandikishe ndugu mpendwa kwa kufungua kurasa hii: http://sw.wikipedia.org/wiki/Special:UserLogin Ukiwa na swali uliza tu utajibiwa.--Mwanaharakati (majadiliano) 15:27, 27 Machi 2008 (UTC)