Majadiliano:Kiyunani
Mandhari
Ninavyoelewa, Kiyunani na Kigiriki siyo lugha ileile. Angalao siku hizi kuna Watanzania wanaotumia jina la Kiyunani kwa lugha ya Agano Jipya tu (yaani Kigiriki cha kale, au kwa Kiingereza "Koine Greek"), wakati jina la Kigiriki ni kwa ajili ya lugha ya Wagiriki kwa jumla (yaani wakati wowote na mahali popote) au kwa Kigiriki cha kisasa hasa. Mnaonaje?
Kwa sababu, kama kweli, Kiyunani na Kigiriki ni kitu kimoja (ila maneno yalitumiwa nyakati tofauti katika lugha ya Kiswahili), makala hizo mbili ziunganishwe. La sivyo, tofauti zielezwe. --Oliver Stegen 17:33, 19 Machi 2007 (UTC)