Majadiliano:Kipanya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Bwana Mwasapi, unaweza kutueleza kwa nini umechagua jina "panya pori" kutafsiri jina la Kiingereza "mouse"? Ukitaka kutofautisha kati ya "mouse" na "rat" kwa Kiswahili, nafikiri kwamba "panya pori" si chaguo bora. Panya pori linamaanisha "panya anayeishi porini", lakini spishi nyingi za "mouse" hazitokei porini na spishi nyingi sana za "rat" zinatokea porini. Pia, sijui makala nyingine ambamo "panya pori" linatumiwa kumaanisha "mouse". Nimeona tafsiri "kipanya" na "puku". Mimi mwenyewe ninapenda zaidi jina "kipanya". Ukikubali ningependa kusogeza ukurasa huu. Nani ananiegameza? ChriKo (majadiliano) 23:50, 29 Machi 2010 (UTC)