Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Kaizari

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Yowe - nimegundua kwamba maandishi ya neno hilo ni Kaizari, yaani na z, siyo na s (angalia kamusi ya TUKI). Ingekuwa kazi nyingi ya kubadilisha makala zote. Nitajaribu kufanya hatua kwa hatua. Au kuna asiyekubali na marekebisho hayo? --Oliver Stegen 18:39, 6 Januari 2008 (UTC)[jibu]

Je umgeunda wapi?? Nimefuata Biblia Takatifu katika tafisiri isiyo takatifu lakini ya kawaida - tazama Luka 2,1 (hata kama Krismasi imeshpita). --User_talk:Kipala 22:48, 6 Januari 2008 (UTC)[jibu]
Kamusi zote mbili za TUKI zinaandika Kaizari (Kiingereza-Kiswahili ya 1996 na Kiswahili-Kiingereza ya 2001). Ingawa Biblia inatumia Kaisari (zote mbili, Union Version na Habari Njema), kwenye kurasa za Kiswahili mtandaoni napata Kaizari - hata kwenye tovuti ya Bunge (sawa, ukitafuta kwa Google, kaisari ipo vilevile, ila mara nyingi ama siyo Kiswahili ama ni kurasa za wikipedia tu). Pia kifonetiki, wahariri wa TUKI wamefanya vema - neno hutamkwa na 'z' siyo 's'. Nadhani waandishi wa kale wamekosea walipoiga uandishi wa 's' kutoka Kijerumani (Kaiser) au Kiingereza (Caesar) kwa vile 's' katika lugha hizo mbili hutamkwa kama 'z' katika Kiswahili. Ndiyo sababu nimeanza kubadilisha. Hata hivyo, uandishi wa Kaisari haufutwi - ninarejesha tu kwenye makala za Kaizari. Hii ni faida ya wikipedia: Tunaweza kupata zote mbili. Asante kwa kazi njema, na tukazane! --Oliver Stegen 08:22, 7 Januari 2008 (UTC)[jibu]
Vilevile, mahali pa kuzaliwa kwa Mtakatifu Fransisko huandikwa Assisi kwa Kiitaliano bali Asizi kwa Kiswahili. Tuzingatie matamshi ya 's' na 'z' walivyofanya wahariri wa TUKI. Kuna mifano mingi ... --Oliver Stegen 08:42, 7 Januari 2008 (UTC)[jibu]
Oliver basi tuendelee Kitanzania tu - kwa afikiano. Si Kikenya- kwa panga na mawe.
Sidhani ya kwamba watu wanasoma sana kamusi za TUKI lakini wanasoma Biblia. Kamusi hizi zina mambo mengi. Nazitumia kwa elemnti za kikemia lakini nahofia hawakowengi wanaoelewa hadi sasa ninachoandika. Nilipohubiri au kusikia mahubiri nilisikia "Kaisari" jinsi inavyoandikwa. Kifonetiki- sikubali. Kijerumani sawa, lakini Kilatini (ni neno lao!!): Kaisar! Tena Google: "kwenye Kaizari" kwangu yaonyesha 140, "kwenye Kaisari" 953. Lakini wataalamu waheshimiwe - ingawa: siamini ni sawa. --91.62.10.34 10:39, 7 Januari 2008 (UTC)[jibu]
Halafu: kufuatana na en:wiki Nyerere aliandika "Julius Kaisari". Sikuwahi kuiona mwenyewe hivyo siwezi kuthebitisha ya kwamba Nyerere aliandika Z au S. Lakini google kwa Nyerere Julius Kaisari 241, kwa Nyerere Julius Kaizari 33. Eti kama hata mwalimu alipendelea S nani katika Afrika ya Mashariki atashinda Biblia pamoja na Nyerere? LAbda zaidi kosa la TUKI? (makosa yamo kwao).
Kuhusu Assisi/Asizi: hi ni wazi kabisa. Kwa majina ya mahali nimetumia kawaida ya mahali penyewe ila pale ambako kuna kawaida tofauti katika Kiswahili tufate haya. Hii si rahisi. Kuna nchi kadhaa zenye majina ya pekee kwa Kiswahili (Ufaransa...); kwa nyingine ni ama umbo la Kiingereza au kile Kilatini cha kimataifa kinachopatikana kupitia Kiingereza (Mongolia); Lakini miji? Hii ni vigumu. Kuna kawaida kuandika mara nyingi umbo la Kiingereza lakini kuisoma si Kiswahili lakini kwa matamshi ya Kiingereza; yaani kuandika "Rome", "Nile" ila tu kutamka "Rom", "Nail". Kwa mji kama Assisi sioni faida kuswahilisha Kiitalia. Ingeongeza tu ugumu.

--User_talk:Kipala 13:44, 7 Januari 2008 (UTC)[jibu]

Asante kwa upole wako! Hata mimi sitaki kuanza vita ... :-) --Oliver Stegen 20:26, 7 Januari 2008 (UTC)[jibu]