Majadiliano:Julius Nyerere

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nyerere: mafanikio na ukosoaji[hariri chanzo]

Nafurahi ya kwamba Luhaja amechangia habari za maana kuhusu elimu ya Nyerere, kazi yake na jinsi yeye mwenyewe alivyoona siasa yake ya kiuchumi.

Lakini ameondoa pia vipengele vya ukosoaji dhidi ya mwalimu. Hapa ni kamusi elezo kwa hiyo hakuna mashujaa wala wahalifu ni watu tu, habari za watu na maoni juu ya watu (tunaweza kutoa taarifa ya kwamba mtu fulani atazamiwa na watu fulani kama mshujaa au mhalifu kama taarifa hii ni ya maana).

Ukosoaji dhidi ya Nyerere kuwa alitawala kama dikteta na kutoheshimu haki za binadamu hadi sasa ni sehemu ya urithi wake, pamoja na sifa zake. Pia sijui itasaidia nini kuondoa tamko ya kwamba Waislamu wengine humwona kama wakala wa kanisa katoliki. Hivyo ndivyo nilivyosoma na kusikia mara nyingi sijui kama nakosea. Ama twapata maelezo kamili au turudishe maneno yale jinsi yalivyokuwa kama kumbukumbu ya kwamba makala haikukamilika. --Kipala 15:08, 26 Septemba 2007 (UTC)[jibu]

ukosoaji[hariri chanzo]

Sijaondoa tamko la kwamba waislamu humwona kama wakala wa kanisa katoliki ila nimejaribu kuelezac kinamna nyingine kuwa si waislamu wote bali ni makundi maana nina mifano ya waislamu wanaomtukuza huyu mtu!Sina tatizo kuhusu hilo! --LUHAJA