Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Ikuwo

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mazao mapya yanayoingizwa Ikuwo

[hariri chanzo]

Kumekuwa na mwamko wa wakulima katika eneo la Ikuwo kutaka kuwa na mazao mbadala wa zao lao kuu la Pareto ambalo wamekuwa nalo kwa miaka ya nyuma. Kwa sasa Viazi mviringo vimechukua sura mpya, kutoka kuwa ni kwa chakula tu, sasa vimekuwa ni biashara kubwa. Ngano pia imegeuka toka kuwa ni kwa chakula na kuwa ya biashara zaidi.

Miaka ya karibuni parachichi limekuwa zao jipya na limepokelewa kwa kishindo, limekuwa na tija sababu limekuwa na ongezeko ktk kuongeza kipato kwa jamii ya Ikuwo. Miaka miwili iliyopita Ikuwo imepata zao jipya la Macadamia A4, awamu ya kwanza zao hili lilionekana katika kijiji cha Mlengu kwa Mzee Lameck Kyando. Mkulima huyu anasema alichukua Tukuyu. Mwaka 2022 Asifiwe Malila alichukua Macadamia nuts grafted toka LIMA LTD ya Mbozi na kuziotesha Ikuwo ktk locations tatu tofauti. Matokeo chanya yalipelekea miche grafted kuongezwa zaidi.

Sambamba na Macadamia, miche ya Parchia Nuts ilijaribiwa, nayo imeonyesha uwezekano wa kukua na kuzaa. Migomba nayo iko mbioni kuwa zao la biashara siku chache zijazo. 41.59.102.226 14:13, 13 Julai 2024 (UTC)[jibu]