Majadiliano:Dzaoudzi
Mandhari
Mwenzetu asiyeonekana kwa jina amebadilisha majina ya visiwa vya Pamanzi na Mahore kuwa Nyambo Titi na Nyambo Bole. Ingekuwa vema kama anaweza kujitambulisha na kueleza msingi wa mabadiliko haya. Kama anaweza kuonyesha ya kwamba kuna msingi wa kuingiza majina yale angeonyesha pia kwa nini majina ya awali si sahihi yasionyeshwe tena.
Hata hivyo haikuwa vizuri kubadilisha majina jinsi alivyofanya kwa sababu amevunja viungo. Makala ya Mahore na Pamanzi yapo ila tu hakuna viungo tena. Naomba tujitahadhari.
Narudisha hali ya awaki na mwenzetu anaombwa kujieleza. --Kipala 22:50, 13 Novemba 2006 (UTC)