Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Chui

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chui ni mnyama mwindaji anayewinda kimyakimya sana. Ingawa ni mdogo kuliko wanyama wote wa jenasi ya Panthera, chui bado anaweza kuwinda mnyama mkubwa kwasababu ya fuvu lake kubwa lenye taya zenye nguvu. Ukilinganisha na paka mwili wake ni mrefu zaidi na miguu yake ni mirefu. Urefu wa kichwa na mwili wake ni kati ya sm 125 na 165 na mkia wake unakaribia sm 60 mpaka 110. Urefu wa mabega ni sm 45 mpaka 80. Chui dume ni wakubwa 30% zaidi ukilinganisha na jike, kufikia uzito wa kg 37 mpaka 91 ukilinganisha na jike wenye kg 28 mpaka 60. Chui wenye miili mikubwa hupatikana kwenye maeneo yaliyojitenga na wanyama wengine wala nyama hasa toka kwa wale jamii ya paka wakubwa waliozoeleka kama vile simba na chui wakubwa wenye milia,"tigers".

Chui mara nyingi huchanganywa na paka wengine wenye madoa, kama duma na jagwa. Hata hivyo wana mtindo tofauti wa madoa: duma wana madoa ya kawaida yaliyosambaa mwili wote; jaguar wana madoa madogo ndani ya vijimiraba; wakati chui ana madoa ndani ya miduara midogo kuliko ile ya jaguar. Chui ni mkubwa na mwenye misuli zaidi kuliko duma, lakini mdogo kidogo na mwenye misuli kidigo kuliko jaguar. Madoa ya chui ni ya mviringo kwa Afrika Mashiriki na huwa ya mraba kwa kusini mwa Afrika. Chui wameripotiwa kufikia mpaka umri wa miaka 21. Rangi mbalimbali.

Laurent salaam. Umeweka hapa nakala ya aya mbili za makala ya chui, lakini sifahamu sababu. Unaweza kueleza tafadhali? Asante. ChriKo (majadiliano) 15:22, 19 Mei 2019 (UTC)[jibu]