Majadiliano:Bukabwa

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

bukabwa kama yalivyo maeneo mengi ya vijiji vya Tanzania hususani maeneo ambayo hayana utashi wa kisiasa kwa maana kwamba kijiji hiki hadi tunasheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika hakijawahi kupata mwakilishi wa kisiasa katika nyanja zenye maamuzi ambazo pengine zinaweza kusaidia katika juhudi za kuleta maendeleo.Katika jimbo la uchaguzi la musoma vijijini haijawahi hata mara moja mkabwa kugombea ubunge na hivyo kuwa changamoto katika maendeleo kwa wakabwa. Bukabwa kama maeneo mengine inahitaji juhudi za kisiasa ili kuinusuru na mila potovu za kutowasomesha watoto wa kike ambao wengi wao uishia kuolewa wakiwa katika umri mdogo. Kutokana na uamuzi wa serikali kuanzisha shule za sekondari za kata kijiji hiki ambacho ni makao makuu ya kata ya bukabwa inayojumuisha vijij vya bukabwa,kirumi,mmazami na maeneo yanayozunguka vijiji hivi kama mang'ole n.k inayo shule ya sekondari mmazami ambayo inatoa mssada wa kutoa elimu kwa vijana wengi toka maeneo haya ambapo wakabwa hupata elimu.Kumbuka wakabwa hawapatikani tu bukabwa ila maeneo yote ya vijiji hivi kuna wakabwa wengi kuliko jamii zingine japo bukabwa ina jamii kubwa ya wakabwa na ndo chimbuko kuu la mila na desturi za wakabwa. Ukilinganisha na jamii nyingi za kikurya, jamii ya wakabwa inaonekana kuwa na ustahimilivu hususani katika suala zima la haki na utu. bukabwa