Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Biblia

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

nataka kuuliza kuhusu kitabu kitakatifu Naomba muchangie kujadili mada hii inayohusu maneno ya G. A. Buttrick katika kitabu chake cha The Interperters Dictionary Of The Bible katika "Text, NT" Vol. 4 asema: "The NT (new testament) is now known, whole or in part in nearly five thousand Greek MSS (manuscripts) alone. Every one of these handwritten copies differ from every other one.. it is safe to say that there is not one sentence in the NT in which the MS tradition is wholly uniform...... many of them do have theological significance and were introduced into the text intentionally"; ni mimi sijaelewa, au ni yeye amekosea, au ni kweli aliosema? Itakuaje kitabu kama hichi cha kueleza Kitabu kitakatifu kieleze maneno kama haya? Au si kitabu cha kutegemewa hivo? na maneno aliosema si sawa? Bora iwe hivo; maanake yaweza kuwa hata hivi vitabu vitakatifu vinavotumiwa vina makosa?!!! naomba majibu na mchango wenu kwa ajili nina masuali mengi sana yanayonitatiza.

Mpendwa Eddy Albert. Karibu katika wikipedia ya Kiswahili! Asante kwa kusoma kamusi elezo hiyo na kuandika swali la hapo juu. Bahati mbaya, kamusi elezo haiwezi kujibu maswala ya imani. Mtu akiamua kuamini maneno ya Biblia, basi ni amuzi lake. Ukitafuta uhusiano na Mungu usigeukie kamusi wala vitabu vya teolojia. Upande wa sayansi, ninavyoeleza masomo ya Biblia, naweza kusema kwamba: 1. siyo kila sentensi ambayo ni tofauti katika makala za Agano Jipya zilizonakilishwa kwa mikono tangu karne ya pili baada ya kuzaliwa Kristu; 2. tofauti nyingi katika makala hizo ni za herufi tu, labda za sarufi au uchaguzi wa maneno lakini hazina tofauti za kiteolojia. Kwa hiyo, machoni mwangu, maelezo ya Buttrick hayana msingi imara. Hata hivyo inawezekana kuwa alimaanisha mambo mengine. Sijasoma kitabu chake. Ukiwa na maswali mengine ya imani, bora uwaulize Wakristu wenye imani imara karibu na makao yako. Mambo mengi hayawezi kujadiliwa vizuri mtandaoni, afadhali kupata majibu uso kwa uso. Ujisikie huru kuendelea na usomaji wa wikipedia, kuuliza maswali ya kilichoandikwa, na hata kuongeza habari ambazo hazijaingizwa katika kamusi elzo hiyo. Nitafurahi kukutana nawe tena hapahapa, aidha nakutakia kila baraka ya Mungu. --Oliver Stegen 13:30, 24 May 2007 (UTC)

Start a discussion about Biblia

Start a discussion