Mabreka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mcheza mabreka
Mcheza mabreka akionesha moja ya mitindo yake ya kuzungusha panga kimgongomgongo

Mabreka (vilevile Majoka, kutoka Kiing. Breakdance, breaking, b-boying au b-girling) ni aina ya dansi ambayo inachezwa na watu ambao huwa sehemu ya utamaduni wa hip hop. Mtindo huu wa mabreka ulianzishwa mwanzoni mwa miaka ya 1970 na watu wenye asili ya Puerto Rico na Wamarekani Weusi huko South Bronx jijini New York City. Mtindo huu wa kudansi ulianza kushika hatamu sana katika miaka ya 70 mwishoni na 80 yake katika miji mikubwa ya nchini Marekani.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. April, Matthew (2009). Foundation: B-boys, B-girls, And Hip-Hop Culture In New York. Oxford University Press. ku. 125, 141, 153.