Nenda kwa yaliyomo

Lwiindi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Lwiindi ni sherehe ya kila mwaka ya watu wa Tonga wa kusini mwa Zambia. Ni sherehe ya kutoa shukrani kwa miungu kwa mvua nzuri na mavuno bora. Matunda ya mazao mengi huletwa kwa maonyesho. Sherehe hii kwa kawaida huvutia watu kutoka sehemu mbalimbali za nchi na nje ya nchi. Inafanyika katika eneo linaloitwa Gonde, karibu na makazi ya Mtemi Monze katika Wilaya ya Monze. Tarehe za sherehe hii kwa kawaida ni mwishoni mwa juma la kwanza la mwezi wa Julai wakati wa likizo za Siku ya Mashujaa na Siku ya Umoja.[1]

  1. 'Chief Monze' - Monze Educational Fund [1]
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lwiindi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.