Nenda kwa yaliyomo

Laura Secord

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Laura Secord

Secord mwaka 1865
Amezaliwa Laura Ingersoll
(1775-09-13)13 Septemba 1775
Great Barrington, Province of Massachusetts Bay
Amekufa 17 Oktoba 1868 (umri 93)
Village of Chippawa, Ontario, Canada
Nchi Canadian
Ndoa James B. Secord (m. 17971841) «start: (1797)end+1: (1842)»"Marriage: James B. Secord to Laura Secord" Location: (linkback://sw.wikipedia.org/wiki/Laura_Secord)
Watoto 7

Laura Secord (Massachusetts, Marekani, 13 Septemba 1775 - 17 Oktoba 1868) ni shujaa wa Vita ya 1812, anayejulikana kwa mchango wake muhimu katika kuokoa vikosi vya Uingereza kutoka shambulio la ghafula la Wamarekani[1].

Mnamo Juni 1813, Laura Secord alisafiri kwa miguu kwa takriban kilomita 30 kupitia msitu na ardhi ya uadui kutoka Queenston hadi Beaver Dams, Ontario, ili kuwaonya maafisa wa Uingereza kuhusu shambulio lililopangwa na jeshi la Marekani. Tahadhari yake iliwasaidia vikosi vya Uingereza na washirika wao Waindio kuwashinda Wamarekani katika Vita ya Beaver Dams.

Laura Secord baadaye akahamia Canada anapokumbukwa kama shujaa wa kitaifa kwa ujasiri wake na mchango wake katika historia ya nchi.

Maisha ya awali na mchango wa Laura Secord

[hariri | hariri chanzo]

Baba yake Laura Secord, Thomas Ingersoll, aliishi katika Massachusetts na alipigana upande wa Waasi Wazalendo wakati wa Vita vya Mapinduzi ya Marekani (1775–1783). Mnamo mwaka 1795, alihamishia familia yake katika eneo la Niagara la Upper Canada baada ya kuomba na kupokea mgao wa ardhi.

Muda mfupi baada ya kuhamia huko, Laura aliolewa na Mwaminifu James Secord, ambaye baadaye alijeruhiwa vibaya katika Vita vya Queenston Heights mwanzoni mwa Vita vya 1812. Wakati bado anapona mnamo 1813, Wamarekani walivamia Niagara Peninsula, ikiwemo Queenston. Wakati wa uvamizi huo, Laura alipata taarifa kuhusu shambulio lililopangwa na Wamarekani, na tarehe 22 Juni alisafiri kwa siri ili kuwajulisha Luteni James FitzGibbon katika eneo lililokuwa bado chini ya udhibiti wa Waingereza.[2] Taarifa hiyo iliwasaidia Waingereza pamoja na washirika wao Wamohawk kuwashinda Wamarekani waliokuwa wakivamia katika Vita vya Beaver Dams.

Juhudi zake zilikuwa zimesahaulika hadi mwaka 1860, ambapo Edward, Mwana wa Kifalme wa Wales, alipotembelea Kanada alimzawadia mjane huyo masikini pauni 100 (£13,000 kwa thamani ya mwaka 2022) kwa huduma yake.

Hadithi ya Laura Secord imepewa hadhi ya kishujaa nchini Kanada. Kisa chake kimekuwa mada ya vitabu, maigizo, na mashairi, mara nyingi kikiwa kimepambwa kwa mbwembwe. Tangu kifo chake, Kanada imemuenzi kwa kumpa heshima mbalimbali zikiwemo shule zilizotajwa kwa jina lake, makaburi ya kumbukumbu, jumba la makumbusho, stempu na sarafu ya ukumbusho, pamoja na sanamu katika Valiants Memorial huko mji mkuu wa Kanada.

  1. "Appolonia Albelonia Secord". geni_family_tree (kwa American English). Iliwekwa mnamo 26 Machi 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Pennington, Reina (2003). Amazons to Fighter Pilots – A Biographical Dictionary of Military Women (Volume Two). Westport, Connecticut: Greenwood Press. uk. 390. ISBN 0-313-32708-4.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Laura Secord kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.