Nenda kwa yaliyomo

Lango:Ujenzi/Intro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ujenzi wa ghorofa nyingi unahitaji teknolojia ya kisasa
Ujenzi wa ghorofa nyingi unahitaji teknolojia ya kisasa

Ujenzi ni teknolojia ya kujenga nyumba, viwanda, barabara, daraja au hata miji. Ujenzi ni kazi inayohusisha watu wengi na ngazi mbalimbali ya kupanga na kutekeleza. Majengo madogo yajengwa na watu wenyewe kufuatana na maarifa yao bila mpangilio mkubwa. Wajenzi hutumia maarifa ya watu waliowatangulia. Majengo makubwa zaidi huhitaji mpangilio mwangalifu. Mwenye jengo atatafuta kwanza ushauri wa wataalamu. Msanifu atachora ramani. Wataalamu wengine hukadiria mahitaji ya vifaa na gharama za jengo. Vibali vinahitajika.

Wajenzi watakaa na kupanga mahitaji ya muda, pesa, wafanyakazi na mashine. Wahandisi na mafundi wa fani mbalimbali hushirikiana.