Nenda kwa yaliyomo

Lango:Hip hop/Wimbo uliochaguliwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

"California Love" ni wimbo wa hip hop ulioimbwa na 2Pac akishirikiana na Dr. Dre na Roger Troutman. Wimbo ulitolewa ukiwa kama single ya kurudi kwa 2Pac juu ya kutoka kwake jela mnamo 1995. Toleo mashuhuri la remix la wimbo huu limeonekana kwenye albamu-mbili za pamoja ya All Eyez on Me mnamo 1996. Wimbo huu huenda ukawa moja kati ya nyimbo maarufu za 2Pac zenye mafanikio zaidi, kwa kushika nafasi ya kwanza kwenye Billboard Hot 100 kwa majuma mawili (kama Double-A side single pamoja na "How Do U Want It"). Wimbo ulipata kuchaguliwa kwenye Grammy Award kama Rap Bora ya Msanii wa Kujitegemea na Rap Bora Ilioimbwa na Wasanii Wawili (pamoja na Dr. Dre na Roger Troutman) mnamo 1997.

Toleo halisi la wimbo huu halikupatikana kwenye albamu yoyote ya studio ya Shakur, lakini inaweza kupatikana kwenye kompilesheni ya Vibao Vikali vya Shakur. Mlio wa wimbo umechukuliwa kutoka katika wimbo wa Joe Cocker wa "Woman to Woman", na uorodheshaji mistari ya "California knows how to party" -lifanywa katika Wilaya ya Los Angeles na kiitikio kuimbwa na Roger Troutman. Sauti za "In the City of Compton" na miji mingine na "California knows how to party" imechukuliwa kutoka kwa Ronnie Hudson na Street People's "West Coast Poplock". Remix yake imeingiziwa na sampuli ya wimbo wa "Intimate Connection" wa Kleeer uliotungwa na Norman Durham na Woody Cunningham.

Soma zaidi....