Kupigwa risasi kwa Carlos Carson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mnamo tarehe 6 Juni 2020 Carlos Carson, Mwanaume Mwafrika asiye na silaha huko Tulsa, Oklahoma, alivamiwa na kuuawa na mlinzi wa kampuni ya kibinafsi mwenye historia kubwa na yenye utata ya kutekeleza sheria.

Tukio[hariri | hariri chanzo]

Carson alikuwa amekaa kwenye moteli, Knights Inn, kwa siku kadhaa. Mapema alasiri ya Juni 6, Carson alikuwa akitembea kwenye maegesho ya moteli hiyo akiwa na kikombe cha kahawa, wakati huo huo, bila ya onyo, alishambuliwa kwa silaha ya kemikali na kisha kupigwa risasi na kuuawa na mlinzi wa kibinafsi Christopher Straight, kulingana na video ya uchunguzi.[1][2][3][4]Risasi mbili zilimpiga Carson, zote ziliingia kwenye mwili wake na mojawapo ilingia kichwani mwake,[4] Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 53 wakati huo, aliwekwa kizuizini baadaye siku hiyo na Idara ya Polisi ya Tulsa, na mnamo Juni 10 alishtakiwa na mwendesha mashtaka wa Kaunti ya Tulsa kwa kuua bila kukusudia.[1][3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]