Nenda kwa yaliyomo

Kopo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kopo
Kopo iliyofunguliwa

Kopo (ing. tin au can) ni chombo cha metali kinachofungwa kabisa kwa kusudi la kutunza vyakula, vimiminika au vitu vingine.

Kwa kawaida kopo hutengenezwa kwa bati la chuma au alumini.

Chanzo cha kopo kilikuwa mahitaji ya kijeshi ya kuwa na chakula kwa askari kisichoharibika kikitunzwa kwa muda mrefu. Mfaransa Nicolas Appert aliwahi kutambua kwamba chakula kilichopikwa na kutunzwa katika chupa kilichofungwa kabisa haliharibiki. Baadaye Waingereza walitumia kopo za bati badala ya vyupa amabazo zinafaida ya kutovunjika haraka.

Siri ya kutunza chakula kwenye kopo ni kama kinapikwa bakteria zote ndani yake zinazosababisha kuoza zinakufa na kama kopo inafungwa mara moja bakteria nyingine za hewani haziwezi kuingia. Siku hizi kuna pia mbinu nyingine kutunza vyakula katika kopo kama kuvipasha baridi, kutumia mnururisho wa kuioniza na mengine. Hata hivyo, kufisha bakteria kwa joto nimbinu salama zaidi.

Tangu kubuni njia za kutengeneza kopo haraka nyombi hivi vimetumiwa pia kwa kutunza vimiminika kama mafuta au vinywaji.

Viungo vya Nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: